Wednesday, September 18, 2019

MAKTABA YA JAIZMELA: Ben Carson ni nani?


Septemba 18, 1951 alizaliwa daktari na mtaalamu wa nyurolojia na pia mkurugenzi wa Idara ya Nyurolojia kwa watoto katika Hospitali ya John Hopkins nchini Marekani, Ben Carson. 
Jina lake halisi ni Benjamini Solomon Carson. Mnamo mwaka 2008 alitunukiwa na Rais wa Marekani wakati huo George W. Bush medali ya Uhuru. 

Benjamin Solomon Carson alizaliwa katika eneo la Detroit katika jimbo la Michigan. Mama yake, Sonya Carson, aliacha shule akiwa katika daraja la tatu na kuolewa na Robert Solomon Carson, aliyekuwa mchungaji mzee zaidi katika eneo la Tennesee, wakati mama yake Ben akiwa na umri wa miaka kumi na tatu tu. Wakati Carson akiwa na umri wa miaka nane tu, wazazi wake waliachana. Mama Carson aliachiwa kuwalea Benjamin na kaka yake Curtis, yeye mwenyewe. Alifanya kazi katika sehemu mbili au hata tatu kwa mara moja ili aweze kuwatosheleza watoto wake wawili. Mwanzoni Carson alikuwa na maisha magumu shuleni. Hali iliyopelekea kuwa wa mwisho mara kadhaa katika darasa lake. Alikuwa akiitwa majina mbalimbali kutokana na hali hiyo, hivyo ikapelekea kukua kwa hasira kali ndani yake. Akiwa amedhamiria kubadilisha maisha ya mtoto wake, mama yake Carson akazuia muda wake wa kuangalia runinga na kumzuia kutoka nje kila siku hadi pale atakapokuwa amemaliza kazi zake za shule kila siku. Mama yake Carson alimtaka Kusoma vitabu viwili kutoka maktaba na kuandika taarifa juu ya vitabu hivyo kila wiki, bila kujali elimu yake ndogo, hata hivyo hakuweza kusoma vitu ambavyo vilikuwa vmeandikwa. Lakini mapema, Carson alimshangaza mwalimu wake na wanafunzi wenzake kutokana na maendeleo yake. Anakumbuka “Ni wakati ule ndipo nilipogundua kuwa sikuwa mpumbavu” anagundua baadae. Carson anaendelea kuwashangaza wanafunzi wenzake na ndani ya mwaka mmoja alikuwa na ujuzi na kuwa katika nafasi ya juu katika darasa lake. Baada ya kugundua kuwa alitaka kuwa daktari wa magonjwa ya akili, Carson alimaliza shule na matokeo mazuri yenye heshima na hivyo alijunga na chuo kikuu cha Yale ambapo alipata shahada yake ya kwanza katika maswala ya saikolojia ya akili. Pschology. Baada ya kutoka Yale, aliendelea na shule ya udaktari ya michigan, ambapo hapo ndipo nia yake ya kuwa daktari wa magonjwa ya akili ilipobadilika na kuwa daktari wa mishipa. Uwezo wake mkubwa wa kuona na uwezo wake wa kufikiri haraka ulimfanya awe daktari wa upasuaji mzuri zaidi Baada ya kumaliza shule yake ya udaktari, alikuwa daktari wa mishipa msaidizi katika hospitali ya Johns Hopkins katika jimbo la Baltimore. Akiwa na umri wa miaka 33, alikuwa profesa wa hospitali na pia mkurugenzi wa idara ya upasuaji mishipa ya watoto.


0 Comments:

Post a Comment