Robert Mugabe alizaliwa Februari 21,1924 katika kijiji kilichokuwa karibu na mji mkuu wa
sasa Harare, wakati huo ukijulikana kama Salisbury; na kufariki dunia Septemba 6, 2019 nchini Singapore.
Alisomea taaluma ya ualimu
na anaaminika kuwa na jumla ya shahada saba kutoka vyuo vikuu. Mwanasiasa huyo
alipata umaarufu mkubwa kwa mara ya kwanza pale alipoongoza vita vya msituni
dhidi ya wakoloni walioitawala Zimbabwe, wakati huo ikijulikana kama Rhodesia.
Mugabe alikamatwa na kufungwa jela kwa kipindi cha miaka kumi kufuatia hotuba
aliyoitoa manamo mwaka wa 1964, iliyowagadhabisha wakoloni ambao waliitaja kuwa
ya uchochezi. Aliachiliwa kutoka jela mnamo mwaka wa 1974 na kuingia kwenye
siasa za kushinikiza Waingereza kusitisha utawala wake kwa Rhodesia. Baadaye
Mugabe alitorokea nchi jirani ya Msumbiji na kurudi Rhodesia mnamo mwaka wa
1979. Baada ya Zimbabwe kupata Uhuru wake mwaka wa 1980, Mugambe alichuka
nafasi ya waziri mkuu, na kwendelea kuongoza nchi hiyo chini ya chama tawala
cha Zanu PF. Katika miaka ya mwanzo wa uongozi wake, Mugabe alisifika kwa
upanuzi wa miundo msingi na huduma za kijamii, zikiwepo hospitali na shule za
nchi hiyo. Hali kadhalika, alishutumiwa kwamba aliwanyanyasa wapinzani wake,
wakiongozwa na kiongozi wa upinzani wa wakati huo, Joshua Nkomo. Tume ya kanisa
katoliki kuhusu haki na amani ilitoa ripoti iliyodai kwamba Zaidi ya watu
20,000 walipoteza maisha yao chini ya utawala wa Mugabe. Mugabe alichukua
wadhifa wa urais mnamo mwaka wa 1987 baada ya nafasi ya waziri mkuu kuondolewa
rasmi. Tangu wakati huo ameshinda uchaguzi mara nyingi licha ya kutajwa na
wapinzani wake na waandgalizi mbali mbali kama uliojawa na udanganyifu na
usiokuwa wa haki na kweli. Mke wake wa kwanza, Sally Hayfron, mzawa wa Ghana,
alifariki mnamo mwaka wa 1992 kutokana na ugonjwa wa figo. Mugabe alimuoa mkewe
wa sasa, Grace Mugabe, mnamo mwaka wa 1996. Wakososaji wa rais huyo walitaja
hatua yake ya mageuzi juu ya umiliki wa ardhi kama moja ya masuala muhimu
yaliyochangia hali ya kuzorota vibaya kwa uchumi wa nchi hiyo. Aidha,
mwanasiasa huyo mkongwe amekosolewa kwa kile wapinzani wake walikiita kukatalia
madarakani, kuwanyanyanyasa wapinzani wake wa kisiasa, kumfuta kazi makamu wake
na kuunga mkono azima ya mkewe ya kutaka kuwa rais wa Zimbabwe, kati ya mambo
mengine yaliyozua utata.
0 Comments:
Post a Comment