Tuesday, September 24, 2019

Museveni akutana na viongozi wa dini Kampala

Rais Yoweri Kaguta Museveni amekutana na wachungaji na wainjilisti wa makanisa ya kilokole jijini Kampala. 

Katika Mkutano huo umefanyika Museveni amewataka viongozi hao wa dini kuisaidia serikali kupambana na umaskini kwa kushiriki katika kujenga maeneo ya kibiashara ambayo yatasaidia kuwainua watu kutoka katika umasikini.

Museveni amesisitiza kuwa ameziona sekta saba muhimu ambazo kanisa linaweza kusimama nazo kwa ajili ya kuwatoa watu katika umaskini ikiwamo uvuvi, kilimo cha kahawa, kilimo cha matunda, kilimo cha ndizi, ufugaji wa kisasa wa mifugo ikiwamo kuku. 

Hata hivyo Museveni amesema anapendelea kuwaona watu wakilima miwa, mahindi na pamba katika mashamba makubwa. Kwa upande wao wachungaji hao wamemuomba kiongozi huyo kuingilia kati muswada ambao ukipita utawazuia wachungaji wasio na elimu ya Biblia kusimama madhabahuni.

Mkutano huo umefanyika katika Uwanja wa Kriketi wa Kampala ambako wachungaji hao katika tamko lao la pamoja walimuomba Museveni aingilie kati muswada huo ambao unapigiwa kelele na watu wengi nchini humo. Zaidi ya wachungaji 50,000 walialikwa kutoka wilaya zote nchini humo.


CHANZO: NEW VISION

0 Comments:

Post a Comment