Saturday, September 7, 2019

MAKTABA YA JAIZMELA: Abdurrahman Wahid ni nani?


Septemba 7, 1940 alizaliwa Rais wa zamani wa Indonesia Abdurrahman Wahid maarufu kwa jina la Gus Dur. 

Alizaliwa katika mji wa Denanyar, Java ya Mashariki nchini Indonesia wakati huo ikiitwa Dutch East Indies. Gus Dur alifariki Desemba 30, 2009 jijini Jakarta nchini Indonesia. 

Gus Dur alikuwa kiongozi wa dini ya kiislamu na mwanasiasa mabaye aliiongoza Indonesia kwa kipindi cha miaka mitatu kutoka mwaka 1999 hadi 2001. 

Mababu wa Gus Dur walikuwa miongoni mwa waanzilishi wa Nahdatul Ulama (NU) miongoni mwa oganaizesheni kubwa ya kisslamu inayokadiriwa kuwa na waumini akali ya milioni 25. Gus Dur aliisoma Qur’an kwa kina akiwa katika shule ya bweni huko huko Java Mashariki iliyoanzishwa na babu yake upande wa baba yake Hasyim Asy’ari. 

Pia alipata fursa ya kuisoma Qur’an alipokuwa katika taasisi jijini Jakarta wakati ambao baba yake alikuwa mjumbe katika bodi ya kidini. Mnamo mwaka 1965 alipata ufadhili wa kwenda kusoma katika Chuo Kikuu maarufu ulimwenguni cha Azhar kilichopo jijini Cairo, Misri. 

Akiwa hapo alitarajiwa kama angechukua masomo ya kiutamaduni kuhusu dini yake lakini aliyatupa nje na kuanza kusoma masomo ya filamu na lugha ya Kifaransa na Kiingereza pia falsafa za Marx. 

Aliondoka Azhar bila kupata shahada yoyote. Gus Dur alienda zake Baghdad, Iraki na kuwavutia tena watu mbalimbali kutokana na maandiko yake ya kidini. Baada ya kurudi nchini Indonesia mwishoni mwa miaka ya 1960 Gus Dur alipata cheo cha kuwa mwenyekiti wa Ulama nafasi aliyoipata mwaka 1984. 

Taasisi hiyo ya Ulama ilijikita pia katika siasa na masuala ya kijamii ikiwamo elimu. Ilikuwa ikipinga baadhi ya mienendo ya serikali huku ikisimamia kauli mbiu ya ‘Songa mbele katika kuibadili jamii kijamii na kiutamaduni.’  

Kutokana na mgogoro wa kiuchumi uliolikumba taifa hilo la Indonesia mwaka 1997-98 wakati wa utawala wa Suharto, Gus Dur na wenzake walishinikiza Suharto ajiuzulu na yeye akachaguliwa mwaka 1999 kuliongoza taifa hilo. 

Gus Dur aliweka rekodi ya kuwa mtu wa kwanza kuwania nafasi hiyo na kushinda kwa kura na aliondoka madaraka kwa kura ya kutokuwa na imani mnamo mwaka 2001. Hata alipoondoka madaraka aliendelea kusisitiza amani ya dunia.

0 Comments:

Post a Comment