Septemba 26, 1965 alizaliwa
mwanasiasa na mfanyabiashara wa Ukraine ambaye alikuwa Rais wa tano wa taifa
hilo, kati ya mwaka 2014 hadi 2019.
Alizaliwa mjini Bolhrad wakati huo ikiwa
sehemu ya Urusi ya zamani (USSR). Baba yake alifahamika kwa jina la Oleksij
Poroshenko alikuwa mhandisi na baadaye alikuja kuwa afisa wa serikali ambaye
alisimamia viwanda mbalimbali katika USSR eneo la Ukraine. Mama yake
alifahamika kwa jina la Yevguenia Grigorchuk ambaye alizaliwa 1937 na kufariki
dunia mwaka 2004 alikuwa ni mhasibu ambaye alikuwa akifundisha katika shule za
ufundi. Poroshenko alikulia katika mjini Bendery ambako baba yake alikuwa
akijenga kiwanda. Tangu akiwa mtoto alikuwa akicheza sana za mapigano katika
Judo na Sambo. Licha ya kuwa na matokeo mazuri katika michezo hiyo lakini
hakupewa medali ya dhahabu wakati akihitimu masomo yake kutokana na tabia yake.
Baada ya kupambana na wanajeshi wa Kisoviet na kuwashinda alipelekwa katika
jeshi huko Kazakh ambako ilikuwa sehemu ya Umoja wa Kisoviet. Mnamo mwaka 1989
Poroshenko alihitimu shahada yake ya uchumi katika masuala ya Kimataifa katika
chuo kikuu cha Kiev. Wakati akisoma masomo hayo alisoma na Rais wa zamani wa
Georgia na Gavana wa Mkoa wa Oder Blast Mikheil Saakashvili. Poroshenko alimwoa
mwanafunzi wa masuala ya udaktari mwaka 1984 Maryna Perevedentseva ambaye
alikuwa amemzidi miaka mitatu na kufanikiwa kuzaa watoto watatu. Katika siasa
Poroshenko amewahi kuwa Waziri wa Masuala ya Kigeni kati ya mwaka 2009 na 2010
pia Waziri wa Biashara na Maendeleo ya Uchumi mwaka 2012. Kutoka mwaka 2007
hadi 2012 Poroshenko alikuwa Mkuu wa Baraza la Benki Kuu ya Ukraine. Poroshenko
amekuwa miongoni mwa wafanyabiashara wenye mafanikio makubwa na vitega uchumi
nchini Ukraine. Mei 25, 2014 alipita katika duru ya kwanza ya uchaguzi akipata
asilimia 54.7 ya kura, ushindi huo ulimfanya asiende katika duru la pili katika
kinyang’anyiro hicho. Katika kipindi cha
pili Poroshenko alishindwa mbele ya mchekeshaji Volodymyr Zelensky akipata
asilimia 24.5 ya kura katika duru la pili la kinyang’anyiro hicho.
0 Comments:
Post a Comment