Septemba 11, 1965 alizaliwa
Rais wa sasa wa Syria na Amiri jeshi mkuu wa vikosi vya jeshi la Syria, Katibu
mkuu wa chama tawala cha Ba’ath na Katibu wa Kanda wa tawi la chama hicho
nchini humo Bashar Hafez al-Assad.
Alizaliwa mjini Damascus katika familia
maskini. Baba yake aliyefanikiwa kufufua Tawi la Chama cha Kiarabu cha Kisoshalisti cha Ba’ath nchini Syria ambapo baada ya mapinduzi
ya mwaka 1970 aliingoza nchi hiyo. Ufanisi
na umakini wa Hafez al-Assad katika historia ya Syria kama kiongozi ndiyo uliompa jina la Simba
katika mataifa ya Kiarabu. Alipata elimu
ya msingi na sekondari katika shule
yenye mchipuo wa lugha za Kiarabu-Kifaransa
ya Al-Hurriya katika mji wa Damascus. Mwaka 1982 alihitimu sekondari na
kwenda kusomEa ufamasia na matibabu katika Chuo Kikuu cha Damascus. Mwaka 1988,
Bashar al Assad alihitimu kozi hiyo
na kufanya kazi kama daktari katika
hospitali ya Jeshi “Tishrin” iliyoko nje kidogo ya mji wa Damascus. Miaka minne baadaye,
alikwenda Uingereza kuanza mafunzo
shahada ya uzamili Kitengo cha Ophthalmology
katika Hospitali ya Western Eye sehemu ya hospitali za kufundishia za
St. Mary jijini London. Bashar Al Assad
wakati huo alikuwa hana matarajio
makubwa ya kuwa mwanasiasa ambapo kaka
yake, Bassel al-Assad, alitarajiwa kama rais wa baadaye, lakini hakutangaza
dhamira hiyo. Mwaka 1994, Rais Bashar
aliitisha kikao cha na jeshi baada ya
kifo cha kushtukiza cha kaka yake,
Bassel kilichosababishwa na ajali ya gari. Muda mfupi baada ya kifo cha
Bassel, Hafez Assa, baba wa Rais wa Syria
alimtangaza Bashar Al Assad kama mrithi wa Utawala wake. Rais Bashar
Assad aliandaliwa utaratibu maalum wa kutambulishwa uliokuwa katika awamu tatu.
Kwanza alimpeleka jeshini, pili picha yake ilitambulishwa kwa umma na tatu
alikaimu madaraka kama kiongozi wa Syria baada ya kifo cha baba yake mwaka
2000. Baada ya kifo cha baba yake, mwaka 2000 Bashar aliteuliwa kuwa kiongozi
wa Chama cha Ba’ath na Jeshi, na alichaguliwa kuwa rais bila kupingwa katika
Bunge la nchi hiyo kwa kupata asilimia 97.2 ya kura. Sanjali na kazi yake ya kijeshi, Bashar alikuwa
mshiriki mkubwa katika masuala ya umma. Alipewa mamlaka kubwa kama mshauri wa
kisiasa kwa Rais Hafez al-Assad, mkuu wa ofisi ya kupokea malalamiko ya rufaa
ya wananchi, na pia aliongoza kampeni dhidi ya rushwa. Mei 27, 2007 Bashar aliapitishwa kama rais kwa
kipindi kingine cha miaka saba, pamoja na matokeo rasmi ya asilimia 97.6 ya
kura za maoni. Baada ya kushika madarala alibadilisha maisha ya watu wa Syria
tofauti ya wakati wa baba yake kisiasa na kiuchumi. Bashal al Assad amekuwa na
uhusiano wa karibu na mataifa ya China na Urusi kutokana na uwekezaji mkubwa wa
mafuta ndani ya nchi yake, lakini pia uhusiano mdogo na uliotetereka kwa
jumuiya ya nchi za kiarabu na mataifa ya Magharibi. Kutokana na upepo wa
mabadiliko katika mataifa ya kiarabu
ulioanzia Tunisia, Serikali ya rais Bashar al Assad haikusalimika katika mabadiliko hayo. Januari 26, 2011 Wasyria
waliandamana kupinga uongozi wake. Wito wa waandamanaji hao ni kutaka mageuzi
ya kisiasa na kurejeshwa kwa haki za
kiraia, pamoja na kuondolewa kwa sheria ya hali ya hatari ambayo imedumu tangu
mwaka 1963. Mnamo Juni 2014 Assad alikuwa kwenye orodha ya maofisa wa serikali
ulimwenguni waliokuwa wakitafutwa kwa uhalifu wa kivita na mahakama ya
Kimataifa ya Uhalifu wa Kivita ya ICC. Assad aliitolea nje mahakama hiyo na
kuikosoa serikali ya Marekani kwa kuingilia masuala ya ndani ya Syria. Assad
anaongea lugha ya kiingereza vizuri na kifaransa kile cha kuongea. Alipokuwa
katika shule ya Al Hurriyah jijini Damascus alijifunza Kifaransa na Kiarabu.
Desemba 2000 alimwoa Asma ambaye ni raia wa Syria mwenye asili ya Uingereza
pale Acton jijini London. Mnamo mwaka 2001 mkewe alimzaliwa mtoto wa kwanza
ambaye alimwita Hafez likiwa ni jina la babu yake. Hafez al-Assad. Mnamo mwaka
2003 alimzalia tena mtoto wa kike waliyempa jina la Zein na mwaka 2004
alizaliwa Karim.
0 Comments:
Post a Comment