Aliyekuwa Mhariri wa
Gazeti la Jamhuri, Godfrey Dilunga, amefariki dunia usiku wa kuamkia Jumanne
Septemba 17, 2019, katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), Dar es Salaam,
alikokuwa akipatiwa matibabu.
Mwili wake unasafirishwa kwenda Morogoro leo
Septemba 18, 2019, na msiba uko Kimara Stop-Over jijini Dar es Salaam kwa dada
yake. Kwa mujibu wa Kampuni ya Jamhuri Media Limited ambako alikuwa akifanyia
kazi, kifo cha mfanyakazi wake, Godfrey Dilunga kimetokana na maradhi ya tumbo.
Dilunga alilazwa katika hospitali hiyo ya Taifa Muhimbili (MNH) Septemba 9,
mwaka huu akitokea katika Hospitali ya Mwananyamala kwa rufaa.
Katika taarifa
iliyotolewa na Jamhuri Media, kwa sasa maandalizi ya kuuaga mwili wa marehemu
Dilunga jijini Dar es Salaam yanafanyika na kisha utasafirishwa kesho Septemba
18 kwenda mkoani Morogoro kwaajili ya mazishi.
Dilunga aliajiriwa JML tangu
Februari 1, 2019 kama Mhariri wa Gazeti la JAMHURI ambako amefanya kazi hadi
mauti yalipomfika. Kabla ya kujiunga JAMHURI, Dilunga amepata kufanya kazi na
Gazeti la Raia Mwema na Mtanzania.
Viongozi mbalimbali na wanasiasa wametuma
salama zao za rambirambi kwa ndugu, jamaa na wanatasnia ya habari kwa msiba
huo.
0 Comments:
Post a Comment