Kenya ni taifa ambalo ni 48 kwa ukubwa duniani
likiwa na kilometa za mraba 580,367.
Kwa makadirio ya mwaka 2019 idadi ya watu
imekifikia milioni 49,364,32 ikiwa ni ongezeko la takribani watu milioni 11
ikilinganishwa na sense ya watu na makazi ya makazi ya 2009.
Pia taifa hilo ni
la 28 kwa kuwa na idadi kubwa kote ulimwenguni. Mji Mkuu ni Nairobi lakini wana
miji mingine maarufu kama Eldoret, Nakuru na Mombasa. Mombasa ni mji wa pili
kwa ukubwa nchini Kenya ukifuatiwa na Kisumu.
Kenya inapakana na Sudan ya Kusini
kwa upande wa Kusini Magharibi; upande wa Kaskazini inapakana na Ethiopia,
upande wa mashariki inapakana na Somalia, upande wa magharibi na Uganda Upande
wa Kusini inapakana na Tanzania na
Kusini Mashariki taifa hilo lililopata uhuru wake mwaka 1963 linapakana na
bahari ya Hindi.
Uchumi wa Kenya ni mkubwa katika Afrika Mashariki na Kati ikilinganishwa
na mataifa mengine katika ukanda huo. Asili ya jina Kenya imetokana na mlima
Kenya. Mpelelezi wa Ujerumani Johann Ludwig Krapf alipowasili katika ardhi hiyo
mnamo karne ya 19 aliwakuta wenyeji wa eneo hilo ambao ni Wakamba.
Chifu wa Wakamba
wakati huo alikuwa Kivoi ambaye alimwongoza Krapf kufika katika kilele cha
mlima huo ambao wenyeji walikuwa wakiutamka kama Ki-nyaa huenda ilitokana na
namna mwamba mweusi na theluji iliyokuwapo walikuwa wakiifananisha na manyoya
ya Mbuni.
Wakikuyu ambao walikuwa wakiishi katika miteremko yam lima Kenya
walikuwa wakiuita mlima huo Kirima Kirinyaga, wakati wale Wa-Embu walikuwa
wakiuita Kirenyaa lakini majina yote matatu yalikuwa na maana moja. Katika
siasa za nchi hiyo Kenya ni nchi ya kidemokrasia ikiwa na mfumo wa vyama vingi
ambapo Rais wa taifa hilo ndiye Mkuu wa Nchi na Serikali.
Imetayarishwa na Jabir Johnson…….Septemba 24, 2019.
Imetayarishwa na Jabir Johnson…….Septemba 24, 2019.
0 Comments:
Post a Comment