Serikali imesema haitaweza
kuufanyia ukarabati uwanja wa ndege wa Moshi kutokana na idadi ndege ya wateja
wanaoumia ukilinganisha na viwanja vingine nchini.
Hayo yalizungumza na Naibu Waziri
wa Maliasili na Utalii Constantine Kanyasu hivi karibuni katika mkutano wa wadau wa
utalii kanda ya kaskazini uliofanyika katika Ofisi za Mkuu wa Mkoa Kilimanjaro mjini
Moshi.
Kanyasu alisema Kanda ya
Kaskazini kwa asilimia zaidi ya 80 inasaidia katika kukuza utalii hasa ikizingatiwa
watalii wengi wanaoingia nchini wamekuwa wakivutiwa na vivutio vilivyoko.
Aidha Kanyasu alisema, “
Ukarabati wa Uwanja wa Ndege wa Moshi unaweza kufanyika endapo tu idadi ya watu
inadhirisha, ukiangalia ndege inaweza kutua hapo ina abiria wawili tu hali
ambayo inakwaza kuutazama ukilingalisha na viwanja vingine nchini.”
Naibu Waziri huyo
alisisitiza kuwa umbali uliopo kati ya Uwanja wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA)
na ule wa Arusha ni mfupi mno hivyo mteja anaona afadhali kukodi basi au taxi
limpeleke kwa ajili ya kwenda kwenye vivutio.
Hata hivyo Kanyasu aliongeza
kwamba Serikali itaanza kuungalia upya endapo idadi ya wateja itaongezeka
katika uwanja huo.
Katika mkutano huo wa wadau
wa Utalii uliongozwa na Mwenyekiti ambaye ni Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Dkt.
Anna Mghwira ambao ulihudhuriwa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo na viongozi
wengine serikali kutoka Uhamiaji na Polisi.
Kwa upande wake Mkuu wa
Mkoa wa Arusha alisema sekta ya utalii inapaswa kuangaliwa kwa jicho la tofauti
kutokana na mwaka wa fedha wa serikali na muda ambao watalii wanaingia kwa
wingi ambao ni mwezi Machi, hali ambayo imekuwa ikizidisha changamoto katika
sekta hiyo.
Gambo alisisitiza serikali imeanza
kuiangazia kwa umakini sekta hiyo katika kanda ya kaskazini ili kuondoa
changamoto zilizopo kwani utalii uliopo katika kanda hiyo ndio unaochangia kukua
mikoa hiyo.
0 Comments:
Post a Comment