Mkoa wa Kilimanjaro umepambwa na Mlima mrefu barani Afrika wenye jina la mkoa huo Mlima Kilimanjaro. |
Mkoa wa
Kilimanjaro ni kati ya mikoa 31 ya Tanzania. Mlima Kilimanjaro, mlima mrefu
kupita yote barani Afrika, umo ndani ya mkoa wa Kilimanjaro. Jina la mlima huu
ndilo limeupatia mkoa jina lake.
Mkoa wa
Kilimanjaro umepakana na Kenya upande wa kaskazini, Mkoa wa Tanga upande wa
kusini na mikoa ya Manyara na Arusha upande wa magharibi.
WAKAZI
Mkoani
Kilimanjaro kuna wakazi wapatao 1,640,087 (sensa ya mwaka 2012). Makabila
makubwa mkoani humo ni Wachagga, Wagweno na Wapare, ambapo pia kuna makabila
mengine madogomadogo kama Wamasai na Wakamba. Makao makuu
ya mkoa huu ni Moshi. Katika sekta
ya elimu wakazi wameendelea kidogo kwa maeneo ya mjini, lakini katika sehemu za
vijijini elimu bado inatetereka kwa kiasi kikubwa, maana teknolojia ya
utandawazi katika eneo kubwa haijashamiri.
WILAYA
Mkoa wa
Kilimanjaro una wilaya 7 ambazo ni: Hai, Mwanga, Moshi mjini, Moshi vijijini,
Rombo na Same na ile mpya ya Siha.
MAJIMBO YA
BUNGE
Wakati wa
uchaguzi mkuu wa Tanzania mwaka 2015 mkoa huu ulikuwa na majimbo ya uchaguzi
yafuatayo:
• Hai : mbunge ni Freeman Mbowe (Chadema)
• Siha : mbunge ni Dk. Godwin Mollel (CCM)
• Moshi Mjini : mbunge ni Jaffary Michael
(Chadema)
• Mwanga : mbunge ni Prof. Jumanne
Maghembe (CCM)
• Same Mashiriki : mbunge ni Nagenjwa
Kaboyoka (Chadema)
• Same Magharibi : mbunge ni Mathayo David
(CCM)
• Moshi Vijijini : mbunge ni Anthony
Calist Komu (Chadema)
• Vunjo : mbunge ni James Mbatia (NCCR)
• Rombo : mbunge ni Joseph Selasini
(Chadema)
0 Comments:
Post a Comment