Nyota wa kimataifa wa Tanzania anayehudumu na Aston Villa ya
Ligi Kuu England, Mbwana Samatta, huenda akatua Galatasaray ya Uturuki
iliyoonyesha nia ya kuhitaji huduma ya mshambuliaji huyo wa zamani wa Simba.
Hata hivyo, Galatasaray inafuatilia mwenendo wa Aston Villa na kwamba iwapo
klabu hiyo itashuka daraja, watatumia mwanya huo kumtwaa Samatta. Samatta aliyejiunga
na Aston Villa Januari mwaka huu akitokea KRC Genk ya Ubelgiji, amefunga mabao
mawili na timu yake hiyo mpya katika mechi za Ligi Kuu England.
Inasemekana
kuwa Galatasaray walikuwa wakimwania Samatta katika kipindi cha dirisha dogo la
usajili la Januari, lakini walipigwa kikumbo na Aston Villa, hivyo kwa sasa
wanajipanga kumnasa usajili wa kiangazi.
Miamba hiyo ya soka Uturuki, inaamini
Villa watakuwa tayari kuwauza wachezaji wao iwapo wakali hao wa England
watashuka daraja.
0 Comments:
Post a Comment