Urembo unajumuisha mambo mengi kwa mwanamke tofauti na
dhana za watu wengi wanaofikiri kwamba urembo ni kuvaa vizuri, kuonekana vizuri
na hata manukato mazuri, kuwa na umbo zuri, na jinsi unavyoonekana kutokana na
umbo lako. La hasha hivi ni vidokezo vya urembo kwa mwanamke.
Urembo halisi ni amani na utulivu uliopo ndani yako,
hali hii ina faida katika moyo wako na mwili wako pia. Jambo la msingi hapa ni
kuwa na amani kwa kuepukana na msongo wa mawazo na kuwa mwenye furaha muda
wote. Hali ya msongo wa mawazo (stress) huleta maradhi mbalimbali kama vidonda
vya tumbo (gastric ulcers), shinikizo la damu (blood pressure) na mengine
mengi.
Katika maisha ya mwanamke yeyote mwenye kupenda urembo
na muonekano mzuri ni pamoja na
kuepukana na magonjwa yanayoepukika kwa njia ya kua na amani na furaha muda
wote kwa kujenga sura nzuri, umbo zuri lenye kupendeza pale unapovaa nguo ya
aina yoyote au kupaka vipodozi vya aina yoyote ile.
Silvia Mushi katika pozi |
0 Comments:
Post a Comment