Aprili 4, 1968 alifariki dunia mwanaharakati wa haki za
binadamu Martin Luther King Jr.
Mike kama ambavyo alipenda kujiita kwa watu
wake wa karibu aliuawa na kundi la wazungu waliochukia harakati zake za
kupigania haki za weusi.
Kijana
aliyetekeleza unyama huu alikuwa ni wa kizungu alijulikana kwa jina la James
Earl Ray huko mjini Memphis, jimbo la Tennessee.
Anakumbukwa kwa hotuba yake maarufu ya ‘I Have a Dream’
yaani Nina Ndoto.
Inaelezwa kuwa aliuawa kwa maagizo ya FBI chini ya Mkurugenzi
katili John Edgar Hoover.
Katika karne ya 20 Mike alikuwa mpambanaji wa
kumkomboa mtu mweusi. Alizaliwa Januari 15,1929 huko Atlanta, Georgia nchini
Marekani.
Alilelewa katika maadili ya dini ya Kikristo hususani madhehebu ya
Baptist.
Hotuba yake ya Agosti 28,1963 jijini New York aliitoa katika Mnara wa
Kumbukumbu wa Rais Abraham Lincoln.
Katika hotuba hiyo alielezea matumaini makubwa
kwa watu weusi akisema ipo siku Wamarekani weusi wataupata Uhuru na Usawa katika
ardhi ya Amerika. (1929-1968)
0 Comments:
Post a Comment