Aprili 1, 1984 alifariki
dunia mwanamuziki, mwimbaji, mtunzi wa nyimbo na prodyuza wa Marekani Marvin
Gaye. Huyu aliisaidia sana kuitengeneza Motown miaka ile ya 1960, katika nafasi
ya mbalimbali za uimbaji lakini baadaye akatuama katika kuchombeza (solo).
Kutokana na umahiri wake katika eneo hilo alipewa majina mengine
maarufu kama “Prince of Motown” na “Prince of Soul.”
Mchana wa Aprili 1, 1984
katika nyumba ya familia huko West Adams jijini Los Angeles, Gaye aliingia
kuamua ugomvi baina ya wazazi wake na baadaye alipambana na baba yake Marvin
Gaye Sr.
Akiwa chumbani kwake majira ya saa 6:38 mchana (PST) baba
yake alimtandika risasi ya kifuani ambayo iliingia katika moyo na kutokezea
katika bega la kushoto. Saa 7:01 mchana (PST) ilitangazwa kuwa Gaye amefariki
dunia. Mwili wake uliwasili katika Hospitali ya California.
Gaye alifariki dunia ikiwa ni siku moja tu ya kumbikizi ya
miaka 45 ya kuzaliwa kwake. Baada ya mazishi ya Gaye mwili wake ulichomwa
katika viunga vya Forest Lawn Memorial
Park huko Hollywood Hills na majivu yake yalitupwa katika bahari ya Pasifiki.
Baada ya kifo chake Baba yake alihukumiwa kwa kesi ya mauaji
lakini baadaye ilipunguzwa hadi kuwa voluntary manslaughter baada ya uchunguzi
uliofanywa katika ubongo.
Marvin Gaye Sr. alihukumiwa miaka sita jela na alifariki
dunia mnamo mwaka 1998 akiwa nyumbani kwake.
Wakati anazaliwa alipewa jina Marvin Pentz Gay Jr. Aprili 2,
1939 katika Hospitali ya Freedman jijini Washington kwa baba yake ambaye
alikuwa mtumishi wa kanisa Marvin Gaye Sr na mfanyakazi wa ndani Alberta Gay.
Gaye alimwoa mwanadada Anna Gordy ambaye alikuwa dada wa
mwanzilishi wa Motown Records Berry Gordy III mnamo June 1963. Wawili hao
walikuwa wadaawa ilipofika mwaka 1973 lakini hati kamili ya kuwa wadaawa
ilitolewa Novemba 1975 na rasmi mahakama ilithibitisha kuachana kwa wawili hao
mnamo mwaka 1977.
Gaye alimwoa Janis Hunter October 1977 lakini wawili wao
waliachana miaka miwili baadaye, rasmi walikuwa wadaawa Februari 1981. Gaye
alizaa watoto watatu. Kazi zake kali akiwa na Motown "Ain't That
Peculiar", "How Sweet It Is (To Be Loved By You)", na "I
Heard It Through the Grapevine".
Pia Gaye alifanya kazi nyingine na Mary Wells, Kim Weston, Diana Ross, na Tammi
Terrell. Mnamo mwaka 1982 alitoa kibao kikali cha "Sexual Healing",
ambacho kilimpa kushinda tuzo mbili za Grammy pamoja na albamu nyingi ya
Midnight Love.
Pia enzi za uhai wake mnamo mwaka 1983 katika NBA All-Star Game
huko Inglewood, California aliimba nyimbo; "The Star-Spangled
Banner"; Motown 25: Yesterday, Today, Forever; na Soul Train na hapo ndio ukawa
mwisho wa kumuona nyota huyo jukwaani.
0 Comments:
Post a Comment