Aprili ni mwezi wa nne wa mwaka katika kalenda ya Gregori na
pia ni mwezi wa tano katika kalenda ya kwanza ya Julian.
Aprili ni mwezi wa
kwanza katika minne ambao una siku 30 na mwezi wa pili katika miezi mitano ya
mwaka ambao una siku chini ya 30.
Mwezi huu unaashiria kumalizika kwa kipindi cha mpito kutoka
majira ya joto kwenda ya baridi. Warumi waliupa mwezi huu jina la Aprilis huku
asili ya neno lenyewe ikiwa bado haijawekwa na bayana. Maana asili ya neno
Aprilis inatokana na kitenzi ‘aperire’ ikiwa na maana ya fungua.
Tafsiri mbalimbali zinasisitiza kuwa kwasababu theluji
ilikuwa imefunika kila kitu katika ardhi; miti na maua yalikua yakianza kutoka.
Pia maana hiyo inaungwa mkono na tafsiri za Wagiriki (Wayunani) wanaotumia neno
Anixi ambalo lina maana ya kufungua lakini wao kilikuwa ni kipindi cha kuanza
kwa majira ya machipuko, joto, autumn na kuanguka kwa theluji katika ardhi.
Hata hivyo kuanzia hapo Warumi waliutaja Aprili kutokana na
sababu za kiroho kwa mungu wao wa kike Venus na sikukuu ya Veneralia ilikuwa
ikiadhimishwa Aprili Mosi ili kumpa heshima mungu huyo waliyeamini kuwa ana
uwezo wa kumtakasa mtu kutoka katika maovu na kumweka katika hali ya nzuri ya
mvuto wa kimapenzi.
Pia walikuwa wakiadhamisha sambamba na mungu Fortuna Virilis
ambaye alikuwa maalumu kwa wanawake.
Sherehe hizi zilianza kuadhimishwa mwaka 220 K.K licha ya
kwamba katikati ya karne ya 4 B.K jina Veneralia ndio lilianza kutumika rasmi.
Watu wa Jamii ya Etruscan waliokuwa wakiishi katika ukanda wa
kale wa Etruria ambayo kwa sasa ni eneo la Tuscany na upande wa Magharibi wa Umbria
na Kaskazini wa Latium nchini Italia waliiuita mwezi huu Apru wakishabihiana na
Wagiriki ambao walikuwa na mungu aliyefahamika kwa jina la Aphros au Aphodite
ambaye alihusika na upendo, uzuri, raha, shauku na uzao.
Aprili ulikuwa mwezi wa pili kabla ya kuongezwa kwa Ianuarius
na Februarius ambayo ni Januari na Februari na Mfalme Numa Pompilius mnamo mwaka
700 K.K Miezi kuwa na siku 30 iliongezwa kutoka 29 za hapo awali ikiwa ni
maboresho ya kalenda ya Julius Caesar iliyoundwa katikati ya miaka ya 40 K.K
0 Comments:
Post a Comment