Kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa na chuo kikuu cha Johns
Hopkins cha Marekani, idadi ya vifo kutokana na virusi vya Corona kote duniani
imezidi elfu 40.
Hadi kufikia jana watu 40,708 waliripotiwa kufariki kutokana
na virusi hivyo, huku watu zaidi laki 8.26 wakithibitika kuambukizwa, na watu
laki 1.74 kati yao wamepona.
Marekani ni nchi yenye maambukizi mengi zaidi kwa kuwa na
watu zaidi ya laki 1.7 walioambukizwa, ikifuatiwa na Italia yenye watu zaidi
laki 1 walioambukizwa.
CHANZO: CRI Swahili
0 Comments:
Post a Comment