Uongozi wa Halmashauri ya
Manispaa ya Moshi mkoani Kilimanjaro, umeridhishwa na ujenzi wa jalala la kisasa (Dampo), ambao unatajwa
kukamilika kwa asilimia 100.
Meya wa Halmashauri hiyo Raymond Mboya, aliyasema hayo baada ya
ziara yake na waandishi wa habari kutembelea eneo linapojengwa dampo hilo na kuridhishwa na ujenzi huo ambapo alisema kwa sasa wanasubiriwa
kukabidhiwa rasmi ili kuanza matumizi ya
dampo hilo.
Mboya alisema Manispaa hiyo
inatekeleza mradi wa ujenzi wa dampo la kisasa ili kuwezesha wananchi kupata
eneo la kutupia taka ngumu ambazo zimekuwa zikizalishwa majumbani na masokoni.
Katika ziara hiyo pia
Mstahiki Meya alitrembelea ujenzi wa miradi mbalimbali inayotekelezwa kwenye
Halmashauri ya hiyo, ikiwemo ujenzi wa mradi wa kituo cha mabasi makubwa ya
abiria unaojengwa eneo la Ngangamfumuni ambacho hadi kukamilika kwake
kitagharimu kiasi cha Sh bilioni 29 huku akionyeshwa kuridhishwa na ujenzi wa
miradi hiyo.
“Kumamilika kwa dampo hili
litakuwa na msaada mkubwa wa kuondosha changamoto ya taka ngumu ambazo
zinazalishwa kwenye maeneo mbalimbali na kukosa eneo la kuhifadhi,”alisema
Mstahiki Meya.
Alisema mchakato wa ujenzi
wa dampo hilo ulianza tangu mwaka 2019,
hadi kukamilika kwake umegharimu kiasi cha zaidi ya Sh bilioni 2 na kwamba
ujenzi wa dampo hilo unasimamiwa na kampuni ya ukandarasi ya Rocktrotinic Ltd.
ya mjini Moshi.
Awali akizungumza msimamizi
wa Jalala la Kisasa (Dampo) Musa Mapunda alisema ujendi wa dampo hilo
umeshakamili na muda mfupi baada ya kupata mitambo ambayo ni sahihi kwa ajili
ya matumizi ya dampo hilo utaanza.
“Tunategemea kuanza matumizi ya jalala letu
muda mfupi baada ya kupata mitambo ambayo ni sahihi kwa ajili ya matumizi ya
dampo letu la kisasa,”alisema Mapunda.
STORY BY: Kija Elias
ALL PHOTOS BY: Jabir Johnson
0 Comments:
Post a Comment