Nembo ya Asian Games 2026 yazinduliwa rasmi



Nembo ya Mashindano ya Michezo barani Asia inayotarajiwa kufanyika mwaka 2026 (Asian Games 2026) imezinduliwa Aprili 1, 2020. 

Mashindano hayo yatafanyika mjini Aicho-Nagoya nchini Japan. Wabunifu akali ya 884 walituma kazi zao kwa Kamati ya Olimpiki barani humo (OCA) ambapo Profesa  Hiroshi Miyashita kutoka Chuo Kikuu cha Aichi-Sangyo aliibuka mshindi  wa shindano hilo. 

Rais wa OCA Sheikh Ahmad Al-Fahad Al-Sabah amepongeza hatua hiyo kuwa ni mwanzo mzuri wa mafanikio ya mashindano hayo.


Post a Comment

0 Comments