Wakati
ambapo mbio ngumu za magari za Dakar Rally zikitarajiwa kuanza kutimua vumbi
Januari 5 mwaka huu Waandaji wa Matukio ya Michezo nchini Ufaransa (Amaury
Sport) wamesema mbio za mwaka huu zitumike kuhamasisha ukombozi wa mwanamke wa
Kisaudi.
Waandaji
hao wamesisitiza kuwa madereva wa Dakar Rally wanapaswa kuzungumza na serikali
ya Saudia Arabia kuhusu uonevu anaofanyiwa mwanamke wa taifa hilo hususani
katika haki ya kuendesha magari.
Mkurugenzi wa Kitengo cha Mipango katika
Shirika la Human Rights Watch, Minky Worden amesema mashabiki, vyombo vya habari
na timu za madereva wa mbio hizo hawatakiwa kufumba macho yao kuhusu uminywaji wa haki kwa wanawake wa Saudi Arabia.
Mbio
hizo zinatarajiwa kuanza kutimua vumbi mjini Jeddah na kumalizika Januari 17
mwaka huuu huko Al Qiddiya ikiwa ni zaidi ya kilometa 7,000.
0 Comments:
Post a Comment