Sunday, January 19, 2020

Yanga yapokea kipigo tena


Winga wa Yanga Deus Kaseke akimiliki mpira mbele ya viungo wa Azam FC katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara ulioshuhudiwa Yanga ikipoteza kwa kichapo cha bao 1-0.
Azam FC imeibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Young Africans katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliochezwa Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Bao pekee la Azam lilipatikana katika dakika ya 25 ya mchezo huo baada ya mlinzi mpya wa Yanga Ally Abdulkarim Mtoni ‘Sonso’ kujifunga wakati wa harakati za uokozi kutokana na mkwaju wa kona uliotupiwa na Bruce Kangwa kuokolewa na mlinda mlango Farouk Shikalo.

Kwa matokeo hayo Azam inajikita katika nafasi ya pili ya msimamo wa Ligi Kuu ikiwa na pointi 32 baada ya michezo 15 alama sita nyuma ya mabingwa watetezi Simba.

Huo ni mwanzo mbaya wa kocha mpya Luc Eymael ukiwa ni mchezo wa pili mfululizo kupoteza baada ya kichapo cha mabao 3-0 kutoka kwa Kagera Sugar Jumatano iliyopita.
Mshambuliaji wa Yanga David Molinga akimimina krosi mbele ya mlinzi wa Azam FC Bruce Kangwa katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara ambao ulimazika kwa Azam kuibuka na ushindi wa bao 1-0. 

0 Comments:

Post a Comment