Januari 1, 2013 alifariki
dunia mwanamuziki wa pop na country wa nchini Marekani.
Jina lake halisi ni
Clara Ann Flower. Alifariki dunia akiwa na umri wa miaka 85 kutokana na maradhi
ya moyo na mapafu. Alizikwa katika makaburi ya El Camino Memorial Park huko San
Diego.
Enzi za uhai wake Patti Page
alikuwa mahiri katika muziki wa pop na country na mara chache alijihusisha na uigizaji.
Alikaa katika orodha ya juu katika chats nchini Marekani kwa mwanamuziki
mwanamke na pia alifanya vizuri sokoni miaka ile ya 1950.
Aliuza kazi zake
ulimwenguni zaidi ya milioni 100 katika kipindi chote cha miongo sita ya
uimbaji wake. Alianza kwa wimbo wa The Singin’ Rage, baadaye akatoa Miss Patti
Page.
Pia inaelezwa kuwa jijini New York kuna DJ mmoja maarufu wakati huo
aliyefahamika kwa jina la Williams B. Williams ndiye alimtambulisha kama ‘A Page
in my life called Patti.’
Patti Page alisaini mkataba wake na Mercury Records
mnamo mwaka 1947 na kuwa mwanamuziki wa kwanza mwanamke kuwa na mafanikio kwa
Mercury Records ambapo mwaka 1948 walitoa albamu ya Confess. Mnamo mwaka 1950
alitoa singo "With My Eyes Wide Open, I'm Dreaming” ambayo ilimuweka
sokoni kwa kuuza kazi hiyo kwa zaidi ya milioni moja.
Wimbo wake wa Tennesse
Waltz pia ni miongoni mwa nyimbo zilizompa umaarufu mkubwa. Baadaye wimbo huo
jimbo la Tennessee liliufanya kuwa wimbo rasmi wa jimbo hilo. Tofauti na
wanamuziki wengine wa pop, Patti Page aliunganisha na vionjo vya country katika
muziki wake.
Mnamo mwaka 1997 Patti Page aliingizwa katika Jumba la Wakongwe wa
Muziki la Oklahoma maarufu Oklahoma Music Hall of Fame na mwaka 2013
alitunukiwa tuzo ya heshima ya Grammy kwa mchango wake katika muziki enzi za
uhai wake.
Alizaliwa Novemba 8, 1927
Claremore katika jimbo la Oklahoma nchini Marekani.
0 Comments:
Post a Comment