Monday, January 27, 2020

Kitambi Noma yatoa dozi yaizabua Moshi Veterans Club 3-2

Moshi Veterans Club wakiwa katika dimba la Ilboru Secondary School jijini Arusha kwenye warm up muda mchache kabla ya kuivaa Kitambi Noma katika mchezo wa kirafiki Januari 26, 2020. (Picha na Johnson Jabir)
 Moshi Veterans Club imeshindwa kutamba katika mchezo wake wa kirafiki dhidi ya Kitambi Noma baada ya kuambulia kichapo cha mabao 3-2 kwenye mchezo uliochezwa katika dimba la Sekondari ya Ilboru jijini Arusha. 

Salehe Salum 'Macheda' alikuwa wa kwanza kuliona lango la Kitambi Noma katika dakika ya 10 baada ya kazi nzuri ya Madesho. 

Abdul Madesho ndiye aliyeisawazishia Moshi Veterans Club katika dakika ya 56 ya baada ya kufumua mkwaju uliokufa mita 27 kutoka katika lango la Kitambi Noma na kufanya ubao kusomeka 2-2.

Hata hivyo dakika ya 73 ya mchezo huo uliokuwa wa kuvutia kutoka na ushindani mkali wa kila upande Sanga Ngomelo alipigilia msumari wa mwisho na kuifanya Kitambi Noma ing'are katika mchezo huo.

Awali Kitambi Nomailifumania nyavu kupitia kwa Muddy Mshana na Kevin Lema katika mchezo huo dhidi ya Moshi Veterans Club.

Mwenyekiti Tumaini Mungete wa MVC alikaririwa akisema, "Asiwepo wa kujitetea, siku zote huwa napenda kusema mchezo una matokeo matatu kushinda, sare na kufungwa, tumekubali wametufunga walikuwa bora kuliko sisi tunawakaribisha Moshi."


Kwa upande wake Msemaji wa Kitambi Noma Ali Msungi alisema mechi hiyo ya kirafiki ilikuwa nzuri na kwamba wameuanza mwaka vizuri hivyo wanaamini katika mechi zijazo licha ya upinzani kuwa mkali watakuwa na matokeo mazuri.

Kikosi cha Moshi Veterans Club mwaka 2020
Kikosi cha Kitambi Noma mwaka 2020



Kocha wa Kitambi Noma akizungumza na wachezaji wake baada ya kipindi cha kwanza kumalizika

Mlinzi wa pembeni kulia wa Moshi Veterans Club Hard Core akiondoa hatari langoni mwake dhidi mshambuliaji wa Kitambi Noma.

Winga wa Kitambi Noma akitafuta njia ya kupita.

Ilikuwa ni kazi kwelikweli baina ya Kitambi Noma na Moshi Veterans Club katika kufungua mwaka 2020

0 Comments:

Post a Comment