Januari 15, 1947 alifariki
dunia mwanadada mhudumu wa Hoteli nchini Marekani aliyefahamika kwa jina la
Elizabeth Short maarufu Black Dahlia.
Mwanadada huyu mrembo aliyezaliwa Julai
29, 1924 alikutwa ameuawa katika viunga vya Leimert Park jijini Los Angeles
katika jimbo la California.
Maiti ya
mwanadada huyo ilipigwa picha na kuandikwa katika magazeti ikionyeshwa kuwa
ilianza kuliwa na wadudu katika sehemu za kiuno.
Mwanadada huyo mwenyeji wa
Boston alikulia Medford, Massachussets
na Florida kabla ya kuweka makazi yake California ambako baba yake
alikuwa akiishi.
Black Dahlia alikuwa akitamani sana kuwa mwigizaji katika maisha yake ya kuishi Los Angeles.
Idara ya Polisi ya Los Angeles
ilianza uchunguzi ambapo watuhumiwa zaidi ya 150 walikamatwa lakini muuaji
hakupatikana. Hata hivyo daktari aliyefahamika kwa jina la George Hill Hodel
alibainika baada ya miaka mingi kuwa ndiye aliyetekeleza mauaji hao.
Daktari huyu alipatikana na makosa ya kumuua
mwanadada Elizabeth Short ambaye alikuwa maarufu kwa jina la Black Dahlia.
Hakuwahi kushtakiwa kwa mauaji hayo. Mwanadada huyo ambaye alikuwa mhudumu wa
hoteli alitangazwa sana katika vyombo vya habari kutokana na mwili wake kukutwa
ukiwa umeharibika sana.
Black Dahlia alifariki dunia Januari 15, 1947 akiwa na
umri wa miaka 22. Kilichosababisha kujulikana kwa muuaji ilikuwa ni mtoto wake
ambaye alisema siku ya msiba wa baba yake kuwa ndiye muhusika mkuu wa mauaji ya
mwanadada Black Dahlia.
Hodel alifariki dunia Mei 16, 1999 akiwa na umri wa
miaka 91. Mtoto wake aliyefahamika kwa jina la Steve Hodel aliwaambia maofisa
wa polisi wa Los Angeles kuwa baba yake aliwahi kufanya mauaji mengine kadhaa.
Kabla ya kesi ya Dahlia, pia alikuwa mtuhumiwa katika kifo cha katibu wake,
Ruth Spaulding, lakini hakushtakiwa. Alishtakiwa pia kwa kumbaka binti yake
mwenyewe, Tamar Hodel, lakini akahukumiwa kwa kosa hilo. Alikimbia nchi mara
kadhaa, na kati ya mwaka 1950 na 1990.
Inaelezwa alikimbia kwenda Ufilipino.
Hodel alizaliwa Los Angeles, California kwa wazazi George Hodel Sr na Esther
Hodel. Wazazi wake walikuwa na asili ya kiyahudi.
Hodel alikuwa mtoto pekee wa
kiume waliyemsomesha na kijana mwenye akili sana. Hodel alikuwa akipendelea
kufanya muziki, alikuwa akipiga kinanda katika matamasha hapo hapo Los Angeles.
Mtunzi wa nyimbo maarufu wakati huo Sergei Rachmaninoff aliwahi kusafiri hadi
nyumbani kwa kina Hodel ili kumsikiliza kijana huyo akiimba.
Alianza kusoma
katika shule ya South Pasadena na alihitimu akiwa na miaka 15. Baada ya hapo
alikwenda katika Chuo cha Teknolojia cha California (Caltech), Pasadena.
Hata
hivyo aliondoka chuoni hapo baada ya mwaka mmoja kutokana na kashfa ya ngono
iliyomhusisha na mke wa Profesa. Hilo halikuwa kosa pekee kwa Hodel kwani
alimtia ujauzito akiwa na malengo ya kuishi naye lakini mwanamke huyo alikataa.
Mambo mengi ya daktari Hodel yalikuja kufahamika baada ya kifo chake. Likiwamo
la kuumua kwa katibu muhtasi Ruth Splauding ili kuficha ukweli kuhusu upotevu
wa fedha katika hospitali na kashfa za utoaji wa mimba ambazo zilikuwa kinyume
na sheria.
0 Comments:
Post a Comment