Kipaji ni kitu ambacho mtu anazaliwa nacho pasipo kufundishwa na mtu yeyote.
Vipo vipaji vingi ambavyo binadamu anaweza kuwa navyo lakini asigundue mapema kuwa amezaliwa na kipaji hicho.Baadhi ya vipaji hivyo ni kuimba nyimbo,kucheza mziki,ususi,uchongaji wa vinyago,kuigiza,kuchekesha nakadhalika.
Ila imekuwa ngumu sana kwa watu wengi kutambua kuwa wamezaliwa na vipaji hivi,na wengi wanakuja kutambua wakiwa wameshakuwa wakubwa.Zipo baadhi ya njia zinazoweza kukusaidia kutambua kipaji chako mapema na ukakikuza na kukiendeleza na mwisho wa siku kikakusaidia kufikia malengo yako katika maisha.
Fanya kile unahisi unaweza kukifanya
Njia ya kwanza kabisa ya kutambua kipaji chako ni kufanya kile ambacho unahisi unaweza kukifanya kwa wakati huo.
Hii itakusaidia sana kujua kipaji chako mapema kwasababu utakapo anza kufanya kile ambacho unahisi unaweza kufanya unaweza kujikuta umefanikiwa zaidi kuliko ungelikaa kimya bila kukifanya.
Kwa mfano kama unahisi unaweza kuimba anza kuimba mapema wakati ukiwa na nguvu na mwisho wa siku utajikuta unakuja kuwa msanii mzuri sana katika hiyo jamii inayokuzungunga.
Wapo baadhi ya wasanii wamejaliwa kugundua kipaji chao mapema na wamefanikiwa kwa kiwango cha juu sana na wanaumri mdogo.
Fanyia mazoezi
Fanyia mazoezi hicho kipaji chako ambacho unahisi Mungu kakujalia.Hakikisha unaanza mazoezi ili uweze kukikuza hicho kipaji chako ambacho mwenyenzi Mungu amekujali.
Mazoezi yataendeleza kipaji chako na kukikuza zaidi kuliko ambavyo ungeamua kukaa kimya bila kufanya mazoezi.
Shirikisha wadau kwenye hicho kipaji chako.
Inapendeza sana kama utawashirikisha wadau mbalimbali hasa wenye kipaji kama chako ili nao waweze kukuongezea baadhi ya vitu katika hicho kipaji chako.
Wadau watakusaidia sana kwa naamna moja au nyingine kukuza kipaji chako kwasababu sapoti yao kwako ni muhimu sana.
Pia unaweza kushirikisha hata mashirika mbalimbali ambayo yanasaidi kukuza baadhi ya vipaji kwenye jamii.
Ondoa Woga
Njia nyingine ni kutokuwa muoga wakati unapoanza kukiinua kipaji chako.
Ukiwa muoga hutaweza kukiendeleza kipaji chako. Unapaswa kuwa jasiri wakati wote na pia uwe mvumilivu kwasababu unaweza ukachukua mda kidogo kukikuza kipaji chako.
Hakikisha unajituma vya kutosha na uoga unauweka pembeni kwani uoga huwakwamisha wengi katika kukuza vipaji vyao.
Uwe mbunifu zaidi.
Ili kukuza kipaji chako unatakiwa uwe mbunifu sana, unapaswa kujiongeza zaidi ili kipaji chako kiweze kukua. Hakikisha unajiongeza kwa wenzako ili uweze kuchukua baadhi ya vitu kutoka kwao na kuviongeza katika kipaji chako.
Kwa kufanya hivi kutakusaidia sana kukiendeleza na kukuza kipaji chako. Ubunifu ndo kila kitu kwenye kiapji chako kama hutakuwa mbunifu zaidi basi itakuwa ngumu kukiendeleza kipaji chako
Mafanikio ni hatua
Usikate tamaa kwa kuwa mafanikio huja taratibu.
Usitake mafanikio ya haraka kwani yanaweza kukukwamisha kwasababu endapo hutafanikiwa mapema basi unaweza ukaamua kuachana na kipaji chako na kufanya mambo mengine ambayo yanaweza yakakukwamisha zaidi.
Hivyo ni vizuri ukawa mvumilivu na ukapambana taratibu na mwisho wa siku utajikuta umefanikiwa zaidi kuliko kutaka mafanikio ya haraka zaidi.
Tafuta kuwa na vyanzo vya Pesa
Unapaswa kuwa na vyanzo vya pesa ili kusaidia kukuza kipaji chako.
Pesa ni kitu muhimu sana katika kukuza kipaji chako kwani unaweza hitaji baadhi ya vitendea kazi ukashindwa kuvinunua kwasababu tu huna fedha za kutosha.Hivyo unapaswa kuwa na vyanzo vya fedha ili viweze kukusaidia.
Vipo vyanzo vingi vya fedha kama vile kuomba marafiki zako au wadau mbalimbali wakuchangie au kushirikisha mashirika mbalimbali ambayo yanaweza kukusaidia kifedha.Pia unaweza ukashirikisha wazazi wako kama wanaweza kukusaidia kifedha.
0 Comments:
Post a Comment