Januari 11, 2005 alifariki dunia mwanamuziki,
mpiga gitaa na mtunzi wa nyimbo wa
Marekani ambaye alifahamika sana katika kategori ya soft rock akiwa na bendi ya
Bread katikati ya miaka ile ya 1970. Huyu sio mwingine ni Jimmy Griffin.
Jina
lake halisi ni James Arthur Griffin. Jimmy alishinda tuzo ya Academy katika
kategori ya Wimbo Bora wa Asili mnamo mwaka 1970. Katika wimbo wa ‘For All We
Know’ alikuwa miongoni mwa walioandika.
Alifariki dunia kutokana na maradhi ya
saratani akiwa nyumbani kwake mjini Franklin huko Tennessee ikiwa ni miezi
kadhaa ya kupatiwa matibabu. Alifariki dunia akiwa na umri wa miaka 61.
Hadi anafariki
alikuwa akiishi na mke wake aliyefahamika kwa jina la Marti, binti zake Katy na
Alexis, watoto wake wa kiume Jamey na Jacob pia wajukuu Laura, Lilli, Gryffn na
Max.
Jimmy alizaliwa Cincinati jimboni
Ohio na alikulia huko Memphis, Tennessee. Mazoezi yake ya muziki yalianza baada
ya wazazi wake kumuingiza katika masomo ya muziki hususani accordion. Alisoma
katika shule ya Kingsbury mjini Memphis.
Wakati akikua katika muziki Johnny
Burnnette na Dorsey walikuwa kioo chake na hakika walimvutia sana Jimmy. Pia
mara kadhaa alikwenda kuwatembelea, hatimaye alifanikiwa kuingia mkataba wa
kurekodi na Reprise Records.
Albamu yake ya kwanza ilikuwa
Summer Holiday aliyoitoa mnamo mwaka 1963. Pia alifanikiwa kuigiza katika
filamu mbili miaka miwili baadaye baada ya kutoa albamu hiyo. Filamu ya For
those who Think Young (1964) na None but the Brave (1965).
Katikati ya miaka ya
1960 Jimmy aliungana na waimbaji wenzake akiwamo Michael Z. Gordon ambaye
alikuwa mahiri sana katika utunzi wa nyimbo.
Wengine ni Ed Ames, Gary Lewis, Bobby Vee, Brian Hyland, The Standells,
Lesley Gore, Sandy Nelson na Cher.
Wote hao walishinda tuzo ya BMI kupitia wimbo wao wa Apologize. Baadaye Jimmy
alikutana na Robby Royer kupitia kwa mkewe Maria Yolanda. Kukutana huko
kulimpeleka katika hatua nyingine ya mafanikio katika muziki.
Mnamo mwaka 1968
Jimmy na Royer wakiwa na David Gates walitengeneza timu ya waimbaji na
kuanzisha bendi mahiri ya BREAD huku wakimtumia mpiga drum Jim Gordon kutoa albamu
yao ya kwanza.
Baadaye Mike Botts alichukua nafasi ya Gordon kama mpigaji wa
moja kwa moja katika bendi hiyo. Gordon alianza kuonekana katika albamu ya pili
ya On the Waters.
Jimmy alizaliwa Agosti 10, 1943
0 Comments:
Post a Comment