Tuesday, January 28, 2020

MAKTABA YA JAIZMELA: Meja Jenerali Suraj Abdurrhman ni nani?

Januari 28, 2015 alifariki dunia mwanajeshi na mhandisi wa majengo wa Jeshi la Nigeria aliyeongoza mapambano katika ardhi ya Liberia Meja-Jenerali Suraj Alao Abdurrahman. 

Mwanajeshi huyo alifariki dunia jijini New York kwa ugonjwa ambao haukuwekwa wazi.

Alisoma shule ya msingi LEA huko Maiduguri Road katika jimbo la Kaduna nchini Nigeria mnamo mwaka 1961 hadi 1967. 

Suraj alifanikiwa kwenda katika vyuo vya serikali kikiwamo cha KEFFI WASC mnamo mwaka 1972. Aliingia katika jeshi la Nigeria mnamo mwaka 1973 na kufanikiwa kuendelea na kozi mbalimbali kuanzia hapo hadi mwaka 1974.

Katika fani ya uhandisi wa majengo alijiunga na chuo cha mnamo mwaka 1976 akaendelea tena katika Chuo Kikuu cha Ahmadu Bello, Zaria kuchukua shahada ya Uhandisi wa Majengo mnamo mwaka 1979. 

Mnamo mwaka 1981 alisalia chuoni hapo na kuchukua Shahada ya Uzamili. Shahda yake ya Uzamivu aliichukulia katika Chuo Kikuu cha Edinburgh huko Uskochi mnamo mwaka 1985. 
Baada ya kuchukua shahada hizo aliendelea kuchukua kozi nyingine za kijeshi ambapo mnamo mwaka 2003 alikwenda katika kozi ya kijeshi ya kimataifa nchini Uingereza Muungano wa Kimataifa. 

Wakati anafariki alikuwa na mke mmoja anayetambulika kwa jina la Fatima Wali-Abdurrahman ambaye walizaa naye watoto wanne Surajudeen, Abduljabbar, Abdulaziz na Abdulmalik. 
Alikuwa akipendelea zaidi kupiga picha , kusafiri na katika michezo alikuwa mpenzi wa gofu na mpira wa kikapu.

Alizaliwa Septemba 9, 1954.

0 Comments:

Post a Comment