Januari 18, 2014 alifariki
dunia mwandishi wa habari na mtangazaji raia wa Ghana aliyefahamika kwa jina la
Komla Dumor.
Mtangazaji huyo wa Idhaa ya Kiswahili wa BBC alifariki nyumbani
kwake jijini London kutokana na maradhi ya moyo ambapo siku moja kabla ya
umauti wake alikuwa studio akifanya kazi.
Rais wa Taifa hilo wakati huo John Mahama aliandika katika akaunti yake ya twitter kuwa Komla alikuwa miongoni mwa mabalozi wazuri na alikuwa matangazaji mwenye ubora usioweza kuelezeka na pia Komla alikuwa zawadi ya Ghana kwa ulimwengu.
Februari 3, 2014 mwili wa mwandishi habari huyo ulisafirishwa kurudi Ghana na kupokelewa katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Kotoka na familia, ndugu, jamaa, marafiki, maofisa wa serikali na wajumbe wa baraza la kijadi la Aflao ambao walisimamia mila na desturi za mjini Aflao.
Sherehe za mazishi zilifanyika kutoka Februari 21 hadi 23 mwaka 2014 jijini Accra. Enzi za uhai wake mwaka 2001 alimwoa Kwansema Quansah ambaye Mwenyezi Mungu alimjalia watoto watatu.
Komla Dumor alianza kama mtangazaji wa kipindi cha asubuhi katika redio Joy FM jijini Accra.
Mnamo mwaka 2003 aliibuka mshindi wa tuzo ya mwaka ya mwandishi wa habari bora ambayo hutolewa na Chama cha Waaandishi wa Habari wa Ghana (GJA). Mnamo mwaka 2006 alijiunga na Idhaa ya BBC upande wa Afrika jijini London ambako alikuwa akishikilia kipindi cha Network Africa.
Kutoka mwaka 2008 hadi 2012 alikuwa akishiriki katika kipindi cha The Wolrd Today hapo hapo BBC. Mnamo mwaka 2011 Komla Dumor alianza kushiriki katika kipindi cha World News na Africa Bussiness Report katika saa za asubuhi.
Mnamo Desemba 2013 jarida la New Magazine lilimtaja katika orodha ya watu 100 wenye ushawishi barani Afrika. Hadi wakati umati unamkuta, mwanahabari huyo alikuwa pekee anayeongoza kutoka Afrika Magharibi katika Idhaa hiyo ya BBC.
Komla Dumor alishawahi kufanya mahojiano na watu wakubwa duniani akiwamo Katibu Mkuu wa zamani wa UN Kofi Annan, Bill Gates na Chimamanda Ngozi Adichie. Pia alionekana katika baadhi ya habari kuhusu Kombe la Dunia mwaka 2010, pia alikuwamo katika msafara wa kufuatilia kwa karibu kuhusu ujio wa Barack Obama barani Afrika na katika mazishi ya mwanaharakati na mwanasiasa Nelson Rohlahla Mandela.
Komla Afeke Dumor alizaliwa Oktoba 3, 1972 jijini Accra kwa baba Ernest Dumor aliyekuwa profesa wa Sosholojia na mama yake Cecelia Dumor alikuwa na shahada ya uzamili katika Mawasiliano ya Umma.

0 Comments:
Post a Comment