Rais Vladimir Putin wa Russia amemteua Mikhail Mishustin kuwa waziri mkuu mpya wa Russia.
Mapema jana baraza la chini la bunge la Russia lilipitisha uteuzi huo kupitia upigaji wa kura.
Baada ya kuteuliwa Mishustin alitoa hotuba kwenye baraza la chini la bunge, na kuwashukuru rais Putin na baraza hilo kwa uungaji mkono wao, pia amesema ataripoti sera za serikali mpya kwa baraza la chini mnamo mwezi Aprili mwaka huu.
Vilevile amewaambia waandishi wa habari kuwa atakabidhi orodha ya mawaziri kwa rais Putin hivi karibuni.
Waziri mkuu wa zamani wa Russia Dmitry Medvedev ameteuliwa kuwa naibu mwenyekiti wa Baraza la usalama la Russia.
0 Comments:
Post a Comment