Polisi Tanzania
imeibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Kagera Sugar katika mchezo wa Ligi
Kuu Tanzania Bara uliochezwa katika dimba la Ushirika mjini Moshi.
Mabao ya Polisi
Tanzania yalifungwa na Sixtus Sabilo kwa mkwaju wa penati na jingine akimalizia
mpira uliotemwa na Benedict Tinoco baada ya mkwaju wa nguvu ulifumuliwa na
Jimmy Mwaisondola.
Bao pekee la Kagera
Sugar lilisawazisha na Kelvin Sabato kwa mkwaju uliokufa nje kidogo ya eneo la
hatari takribani mita 20 kutoka katika lango la kaskazini ambao ulimshinda mlinda
mlango Mohamed Yusuf.
Kwa matokeo hayo
Polisi Tanzania imefikisha pointi 24 ikiwa imecheza 16 huku ikiendelea kusalia
katika 10 bora za msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu 2019/2020.
Kikosi cha Polisi Tanzania
Mohamed Yusuf, Elias
Lucian, Juma Ramadhani, Mohammed Mmanga, Mohamed Kassim, Pato Ngonyani, Sixtus
Sabilu, Jimmy Shoji Mwaisondola, Mohamed Mkopi, Hassan Maulid Mateo Anthony.
Wa Akiba: Kulwa Manzi, Shaban Stambuli, Iddy Mobby, Andrew
Chamungu, Pius Buswita, Erick Msagati, Athanas Mdimu.
Kocha: Malale Hamsini
Kikosi cha Kagera Sugar
Benedict Tinoco,
Mwaita Gerera, David Luhende, Juma Shemvuni, Hassan Isihaka, Peter Mwalyanzi,
Yusuph Mhilu, Ally Ramadhani, Abdallah Sesseme, Awesy Awesu
Wa Akiba: Ramadhani Chalamanda, Juma Nyosso,
Abdulswamad Kassim, Jackson Kibirige, Nassoro Kapama, Jofrey Mwashiuya, Erick
Msagati.
Kocha: Mecky Mexime
0 Comments:
Post a Comment