Friday, January 3, 2020

ATP Cup 2020 vumbi kutimka Brisbane, Perth, Sydney


Msimu wa 2020 Kimataifa katika Tenisi unatarajiwa kuanza kesho Januari 4 ambapo nyota mbalimbali wa mchezo huo wanajiandaa kuanza na mapambano yao kwenye viwanja mbalimbali kwenye mashindano ya kuwania taji la ATP.

Kombe la ATP mwaka huu kwa wanaume linafanyika katika viunga vya vitatu Sydney, Brisbane na Perth nchini Australia ikiwa ni majuma mawili kabla ya kuanza kwa michuano ya Wazi ya Australia maarufu Australian Open (AO).

Mashindano ya ATP yatamalizika Januari 12 mwaka huu ambako kutashuhudia bingwa wa ATP mwaka huu akitangazwa.

Makundi sita yameshapangwa ambapo nyota wa tenisi kutoka mataifa mbalimbali watawakilisha nchi zao, Rafael Nadal ambaye ni nyota namba moja kwa ubora kwa sasa ataiwakilisha Hispania iliyopo katika kundi B pamoja na Japan, Uruguay na Georgia.

Nyota namba mbili kwa ubora Novak Djokovic ameshawasili Brisbane ambako ataiwakilisha  Serbia ambayo ipo kundi A pamoja na Afrika Kusini, Ufaransa na Chile.

Afrika Kusini inawakilishwa na Kevin Anderson ambaye anashika nafasi ya 91 kwa ubora duniani, pia Llyod Harris na Ruan Roelofse

0 Comments:

Post a Comment