Mustapha Dahleb mnamo mwaka 1978 akiwa na PSG |
Januari 8, 1978 klabu ya
Paris Saint Germain (PSG) ya nchini Ufaransa ilibadili mawimbi katika kandanda
la nchi hiyo ikiwa ni miaka minane tu baada ya kuanzishwa kwake pale ilipoweka
rekodi sawa na kuwa na miamba ya siku nyingi Olympique Marseille.
Hapo ndipo kilipozalishwa
kile kinachotwa Le Classique au Derby de France ikiwa ni mechi ya mahasimu wa
Ufaransa.
Kwa mara ya kwanza walicheza
mwaka 1971 na Marseille ilishinda na rekodi hiyo iliendelea kwa misimu mitatu
mfululizo.
Pia Marseille ilikuja
kushinda mchezo wa saba kati ya 11 huku ikipoteza mara moja ambayo ilikuwa
katika Coupe de France mnamo Machi 1975.
Sasa basi katika mchezo wa
mwaka 1978 Marseille walitua katika dimba la Parc des Princes ukiwa ni mchezo
wa 12 ikiwa imeshinda michezo mitatu kati ya nne iliyopita.
Mbele ya watazamaji 33, 386
wageni hao waliendelea kuongoza ambapo dakika ya 12 ya mchezo walipata bao
kupitia kwa nyota wao Sarr Boubacar.
Lakini baadaye PSG
walicharuka na kupata uongozi wa mabao 2-1 yaliyotiwa kimiani na Francois
Brisson katika dakika ya 29 na Mustapha Dahleb katika dakika ya 44.
Katika kipindi cha pili bao
la kujifunga mlinzi wa Marseille Marius Tresor katika dakika ya 46 ilipawa
matumaini makubwa PSG wakiongoza kwa mabao 3-1.
Mshambuliaji wa PSG
Francois M'Pele alifunga dakika tatu baadaye na bao la tano alifunga katika
dakika ya 82 ya mchezo huo hivyo PSG kuongoza kwa 5-1 na ndio yalikuwa matokeo
ya siku hiyo. Hata hivyo ushindi wa mabao zaidi ya manne unakuwa kumbukumbu
tosha katika derby hiyo ambapo Novemba 1986 Marseille ilishinda kwa mabao 4-0.
Hata hivyo Februari 2017
PSG iliibamiza Marseille kwa mabao 5-1. Kuanzia hapo mpaka sasa PSG inaongoza
kwa kushinda dhidi ya Marseille
ikishinda mechi 43 katika michezo 97 waliyokutana huku Marseille
ikishinda mechi 32 na sare 22.
Mwaka 2019 Marseille
ilitandikwa 4-0 hivyo kuongeza idadi ya mechi za ushindi na idadi ya mabao
kufikia 141 huku Marseille wakiwa na mabao 116.
0 Comments:
Post a Comment