Januari 29, 1950 alifariki dunia mtawala wa kumi wa taifa la Kuwait Sheikh Ahmad Al-Jaber Al-Sabah. Alifariki dunia akiwa na umri wa miaka 65.
Sheikh Ahmad Al-Jaber Al-Sabah ni mtoto wa Jaber II Al-Sabah ambaye alikuwa mtawala wa Kuwait kati ya mwaka 1915 hadi 1917.
Aliingia madarakani baada ya kifo cha mjomba wake Salem Al-Sabah ambaye alikuwa mtawala wa tisa wa Kuwait mnamo mwaka 1921 hadi kifo chake.
Baba yake alikuwa kiongozi wa kijeshi na mwanzilishi wa Jeshi la Kuwait pia Mkurugenzi wa Usalama wa Taifa. Miaka ya 1920 aligawa madaraka hayo ya kijeshi kwa Ali Salem Al-Mubarak Al-Sabah na baadaye alichukua Sheikh Abdullah Jaber Al-Abdullah II Al-Sabah kutokana na vita ya Regeai.
Vita hii ilitokea Januari 1928 ambayo inachukuliwa kuwa ndiyo vita ya mwisho katika historia ya awali ya Kuwait.
Pia vita hii ilikuwa ya kwanza katika historia ya Kuwait kutumia magari ya kivita. Ilipiganwa zaidi kaskazini Magharibi mwa mji wa Al Jahra nchini humo wakati wa utawala wa Sheikh Ahmad Al-Jaber Al-Sabah.
Watu kati ya 200 na 300 waliuawa katika mapigano hayo ambayo yalishuhudiwa Kamanda wa Vikosi vya kijeshi Sheikh Ali Salem Al-Mubarak Al-Sabah akipoteza maisha.
Wakati wa uhai wake Sheikh Ahmad Al-Jaber Al-Sabah alioa mara kadhaa na kuzaa watoto saba miongoni mwao ni Nawaf Al-Ahmad Al-Jaber Al-Sabah ambaye ni crown prince wa Kuwait nafasi aliyoichukua mnamo mwaka 2006 hadi sasa.
Sheikh Ahmad Al-Jaber Al-Sabah alifariki dunia katika jumba la Kifalme la Dasman nchini humo.
Alizaliwa mnamo mwaka 1885.
0 Comments:
Post a Comment