Sunday, January 5, 2020

Kariakoo Derby: Simba 2-2 Yanga


 Mechi ya Watani wa Jadi katika soka la Tanzania,  Simba SC na Yanga  wamegawana pointi baada ya sare ya 2-2 katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara jioni ya Januari 4, 2020 Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam.

Kwa sare hiyo, Simba SC inafikisha pointi 35 katika mchezo wa 14, hivyo kuendelea kuongoza Ligi Kuu kwa pointi 10 zaidi ya mahasimu wao hao wa jadi, ambao hata hivyo wamecheza mechi 12 tu.

Balama Mapinduzi aliifungia Yanga bao la kwanza kwa shuti la umbali wa mita 30 baada ya kumpokonya mpira kiungo wa wapinzani, Muzamil Yassin dakika ya 49.

Deo Kanda wa Simba SC alitoka na nafasi yake ilichukuliwa na Hassan Dilunga dakika ya 52 na Mohammed Issa wa Yanga aliyempisha Deus Kaseke dakika ya 69.

Kikosi cha Simba SC kilikuwa; Aishi Manula, Shomari Kapombe, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’, Tairone Santos, Paschal Wawa, Jonas Mkude, Deo Kanda/Hassan Dilunga dk52, Muzamil Yassin, Meddie Kagere/ John Bocco dk69, Clatous Chama na Francis Kahata.

Yanga SC; Farouk Shikhalo, Juma Abdul, Adeyum Ahmed/ Andrew Vincent ‘Dante’dk64, Kelvin Yondan, Ally Mtoni ‘Sonso’, Abdulaziz Makame/ Yikpe Gislein dk62, Mohammed Issa ‘Banka’/ Deus Kaseke dk69, Mapinduzi Balama, Ditram Nchimbi, Papy Kabamba Tshishimbi na Haruna Niyonzima.


0 Comments:

Post a Comment