Tuzo za Shirikisho la Soka barani Afrika zimefanyika jijini
Cairo, Misri kukishuhudiwa Sadio Mane akiibuka mchezaji bora wa Afrika kwa
mwaka 2019 akiwabwaga Mo Salah (Misri) na Riyad Mahrez (Algeria).
Raia huyo wa Senegal na nahodha wa kikosi hicho aliifikisha fainali
ya AFCON 2019. Pia ubora wake kwa mwaka ni mkubwa hususani katika ngazi ya
klabu yake ya Liverpool, akitoa mchango mkubwa wa kutwaa Ligi ya Mabingwa
barani Ulaya.
Mo Salah, Mahrez na Mane wanahudumu katika Ligi Kuu nchini
England.
Aidha tuzo ya timu bora ilikwenda kwa Algeria ambao ndiyo
mabingwa wa Kombe la Mataifa ya Afrika 2019 huku Kocha Djamel Belmadi wa
Algeria akiibuka kocha bora kwa kuinua taji hilo la Afrika.
Tuzo maalum imekwenda kwa mlinda mlango Kodjovi Obilale wa Togo ambaye alishambuliwa
kwenye msafara wa basi wakiwa na timu ya taifa hivyo kupata ulemavu wa kudumu
katika maisha yake. Ndani ya basi hilo alikuwapo mchezaji wa zamani wa Arsenal,
Manchester City Emmanuel Adebayor na mchezaji wa zamani wa Yanga Vincent
Bossou.
Kikosi bora cha Afrika
mwaka 2019:
Andrea Onana (Cameroon), Serge Aurier (Ivory Coast), Joel
Matip (Cameroon), Kalidou Koulibaly (Senegal), Achraf Hakim (Morocco), Igana
Gueye (Senegal), Riyad Mahrez (Algeria), Hakim Ziyech (Morocco), Mo Salah
(Misri), Pierre-Emerick Aubameyang (Gabon), Sadio Mane (Senegal).
0 Comments:
Post a Comment