SDGs: MALENGO YA MAENDELEO ENDELEVU
LENGO NAMBA MOJA - Kutokomeza Umasikini wa Aina Zote Kila Mahali
LENGO NAMBA MOJA - Kutokomeza Umasikini wa Aina Zote Kila Mahali
Lengo hili linahusu kuongeza kipato cha watu
waishio kwenye umaskini na kuhakikisha wanapata huduma za msingi na kumlinda
kila mtu kuepukana na majanga.
Hivyo basi, Serikali za Mitaa zina jukumu la
kuhakikisha kwamba, ifikapo 2030:-
· Zinatokomeza
umasikini uliokithiri kwa watu wote, wanaoishi kwa kipato chini ya dola za
kimarekani 1.25 kwa siku.
· Kiasi cha watu
wanaume, wanawake, na watoto, wa kila umri wanaoishi katika hali ya umasikini
kinapungua japo kwa nusu.
Watu wote, wanawake na wanaume, hasa maskini, wana haki sawa za
kiuchumi na upatikanaji wa huduma za msingi, umiliki wa ardhi na mali
nyinginezo,mirathi, maliasili, teknolojia inayofaa, huduma za kifedha na
mikopo.
· Zinawatambua wananchi
wanaoishi katika hali ya umasikini, ili kuelekeza rasilimali na huduma kwa
wananchi hao kwa ajili ya kuwasaidia kuepuka hali hiyo.
· Zinajenga uwezo
wa watu maskini ili kuwaimarisha na kurekebisha hali yao ya umaskini ili
kuwaondoa katika mazingira yaliyo duni na majanga.
0 Comments:
Post a Comment