Januari 14, 2012 alifariki
dunia mwanasayansi wa Kompyuta au tarakilishi wa Pakistan Arfaa Karim Randhwa.
Alifariki
dunia akiwa na umri wa miaka 16, ambapo mwaka 2011 Arfa Karim alikuwa akisoma
katika Shule ya Lahore Grammar Paragon Campus akiwa katika mwaka wa pili wa
masomo yake ya A level.
Desemba 22, 2011 alipatwa na mshtuko wa moyo baada ya kupata kifafa. Ugonjwa wa kifafa ulisababisha madhara katika ubongo wake hivyo akapelekwa katika hospitali ya kijeshi ya Lahore akiwa katika hali mbaya.
Januari 9, 2012 Mwenyekiti wa Microsoft Bill Gates aliwasiliana na wazazi na madaktari kufanya kila wanaloweza kuokoa uhai wa mtoto huyo. Gates alipeleka timu ya madaktari wa kimataifa ambao waliendelea kuwa na mawasiliano kwa kila kinachoendelea.
Familia ya Randhwa iliomba msaada kwa Bill Gates ambaye alionyesha nia ya kumchukua na kumpeleka nchini Marekani kwa matibabu zaidi. Baba wa mtoto huyo Amjad Adul Karim Randhwa alithibitisha kuwa Gates alikuwa na nia ya dhati kwa ajili ya kumhudumia mtoto wake.
Januari 13, 2012 sehemu ya ubongo wake ilionyesha kuwa na unafuu na kwamba matumaini ya kupaona kwake yalikuwa hai. Hata hivyo Januari 14, 2012 Arfa Karim alifariki dunia akiwa hospitalini mjini Lahore akiwa na umri wa miaka 16 na mazishi yake yalifanyika siku iliyofuata na kuhudhuriwa na Waziri Kiongozi wa Jimbo la Punjab Shahbaz Sharif.
Arfa Karim alizikwa katika makaburi ya kijiji cha Chak No. 4JB Ram Dewali, Faisalabad.
Arfa Karim Randhwa alikuwa mtoto wa kike na mwanasayansi akiwa na umri mdogo. Mnamo mwaka 2004 akiwa na umri wa miaka tisa alikuwa mwanasayansi mwenye umri mdogo ambaye alitunikiwa cheti na kampuni ya Microsoft (MCP).
Akiwa na miaka 10 alipokea leseni ya urubani. Pia jina la Arfa Karim Randhwa limeingia katika vitabu vya rekodi za dunia hususani Guiness Book of World Records.

0 Comments:
Post a Comment