Thursday, September 22, 2016

Jela miaka 4 kwa wizi wa basi la Kanisa



ILALA, DAR ES SALAAM
MAHAKAMA ya Wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam imemhukumu kifungo cha miaka minne jela mkazi wa Ilala Panga Yusuf Mbarouk (42) kwa wizi wa basi la kanisa la Anglikana.
Mbele ya Hakimu Mkazi Adelf Sanchore, Mwendesha Mashtaka Eric Shija alidai mnamo Oktoba 17, 2014 mshtakiwa akiwa na wenzake watatu waliiba gari aina ya Toyota Coaster lenye usajili wa T.379 BBB yenye thamani ya Sh. Milioni 30 mali ya Kanisa la Anglikana, Ilala.
Awali upande wa mashtaka uliteta mashahidi saba akiwamo Padre Thomas Ernest  pamoja na vithibitisho leseni ya gari hilo lenye Chassis Na.1HZB 400003527 na Engine Na. 1HZ0266297, Model Na. HZB40.
Aidha ilidaiwa mahakamani hapo kuwa mshtakiwa ambaye alikuwa mwajiri wa Kampuni la S & M Security Services akiwa na Bahati Mdoe (32), Benard Karoli ‘Master’ (47) na Shaban Msanda (34) walitenda uhalifu huo kinyume na Kifungu cha Sheria Na. 258 na 265 sura ya 16 kilichorekebishwa mwaka 2002 cha kanuni ya adhabu.
Hakimu alisema mahakama imejiridhisha na ushahidi uliotolewa na upande wa mashtaka kuwa mshtakiwa namba moja alitenda kosa hivyo washtakiwa wengine waliachiwa huru.

0 Comments:

Post a Comment