Monday, September 19, 2016

Fundi umeme kizimbani kwa wizi

NA MWANDISHI WETU

FUNDI umeme mkazi wa Kibaha mkoani Pwani Elihood Ruhomvya (37) amepandishwa kortini katika mahakama ya wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam baada ya kukutwa na hatia  ya kutenda makosa mawili kinyume na kanuni za nchi.
Mwendesha Mashtaka Eric Shija mbele ya Hakimu Mkazi Wilberforce Luhwago alidai mshtakiwa alitenda makosa mawili ya kugushi na kuiba kati ya Agosti na Oktoba mwaka 2014 jijini hapa.
Katika kosa la kwanza ilidaiwa mahakamani hapo mshtakiwa aligushi oda za manunuzi zipatazo 31 zenye namba tofauti kwa kutumia saini ya Ashiq Abasi Versi kinyume na Kifungu cha Sheria Na. 333, 335(a) na 337 CAP 168 R.E 2002
Aidha ilidaiwa mahakamani hapo mshtakiwa aliiba wire wenye kipenye cha milimita 2.5 ukiwa kwenye mabunda 117 ukiwa na thamani ya Sh. Milioni 6.3, circuit breaker 23pcs zenye thamani ya Sh. Milioni 2.3, AVs 11pcs zenye thamani ya Sh. Milioni 1.1 na Led Lights 2pcs zenye thamani ya Sh. 29,000 jumla ya mali yote ikiwa ni Sh. 9,654,000 mali ya Clippers Investiment.
Hakimu Mkazi Luhwago alisema masharti ya dhamana yapo wazi kwa mshtakiwa ambaye alitakiwa awe na wadhamini wawili mmojawapo awe mwajiriwa wa serikali na fedha taslimu Sh. 1,500,000.

Shauri hilo litatajwa tena Septemba 22 mwaka huu.

0 Comments:

Post a Comment