NA NEEMA HARRISON, TUDARCO
MAHAKAMA ya Wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam imemhukumu Rashid Mohamed
(32) miaka 30 jela baada ya kupatikana na hatia ya kumbaka mwanafunzi wa miaka
13.
Akisomewa hukumu hiyo jana na Hakimu Mkazi Juma Hassan alisema mahakama
imeridhishwa na ushahidi wa pande zote na kwamba anamtia hatia kutumikia
kifungo hicho.
Awali ilidaiwa na Mwendesha Mashtaka Agatha Lumato mshtakiwa alitenda
kosa hilo maeneo ya Chania Zuala wilayani Ilala, Desemba 13 mwaka jana kinyume
na kifungu cha sheria Na.130(1)(2)(e) na 131(1) sura ya 16 kilichofanyiwa
marekebisho mwaka 2002 cha kanuni ya adhabu
Pia ilidaiwa kuwa mtoto huyo alitumwa dukani kununua mahitaji ndipo
hakuonekana na kwamba mshtakiwa alimfungia muathirika kwa siku 45 huku wazazi
wake wakiwa hawajui mtoto wao alipo na mshtakiwa akiendelea kumfanyia vitendo
viovu.
Aidha ilidaiwa mahakamani hapo kuwa shahidi mmoja ambaye ni jirani wa
mshtakiwa alisema walikuwa wakishangaa kumuona kijana huyo kuishi na mwanafunzi
huyo na muda mwingine kwenda kumuogesha, ndipo walipoamua kutoa taarifa kwa
mjumbe wa Serikali za Mitaa Juma Saidi ambaye alishiriki kukamatwa kwa
mshtakiwa.
Hakimu alisema kupitia ushahidi wa Dk. Joan wa Hospitali ya Amana
jijini Dar es Salaam kupitia vipimo vya kitaalamu umeonyesha mwanafunzi huyo
alikuwa ameathirika vibaya katika sehemu
za siri na tendo hilo limefanyika kwa muda mrefu.
0 Comments:
Post a Comment