Tuesday, September 27, 2016

Kizimbani kwa kukutwa na noti bandia

NA MWANDISHI WETU
Specimen ya Sh. 10,000 ya Tanzania
MKAZI wa Kariakoo jijini Dar es Salaam Mashaka Salum (52) amepandishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala kwa kosa la kukutwa na noti bandia za Sh. 10,000 kinyume na sheria za nchi.
Mwendesha Mashtaka wa Serikali Ashura Mnzava, mbele ya Hakimu Mkazi Wilberforce Luhwago alidai kuwa Agosti 27 mwaka huu saa 3:10 usiku mshtakiwa alikutwa na noti hizo Buguruni Corner Bar, Buguruni Kisiwani kinyume na Kifungu cha Sheria Na. 348 sura ya 16 kilicorekebishwa mwaka 2002 cha Kanuni ya Adhabu.
Ilidaiwa mahakamani hapo noti hizo zenye Na. BT 8486897 kama zingekuwa ni fedha halali zingekuwa na tahamani ya Sh. 90,000.
Hakimu alisema mshtakiwa anaweza kupata dhamana endapo atapata wadhamini wawili kila mmoja awe na Sh. 40,000 na miongoni mwao mmojawapo awe mwajiriwa.
Kesi itatajwa tena Okotoba 10 mwaka huu.

0 Comments:

Post a Comment