NA DIANA JOACHIM, TUDARCO
Washtakiwa wawili wamepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Wilaya ya
Ilala jijini Dar esSalaam kwa kosa la kumbaka msichana wa miaka 15 akiwamo mwanamke mmoja kushirikiana na mbakaji.
Mwendesha mashtaka Eric Shija alidai mbele ya Hakimu Mkazi Wilberforce
Luhwago kuwa siku isiyo na tarehe mwaka huu katika maeneo ya Gongo la Mboto
Samuel Frank (23) ambaye ni mfanyabiashara wa Mtongani jijini hapa
akishirikiana na Fatima Salum 'Mama Mudy' (21) walitenda kosa kinyume na
kifungu cha sheria 130(1),(2)(e) na 131(1) sura ya 16 kilichofanyiwa
marekebisho mwaka 2002 cha kanuni ya adhabu.
Aidha ilidaiwa Frank alimbaka binti huyo na kumsababishia maumivu
makali.
Pia mwendesha mashtaka aliongeza kuwa Mama Mudy alikwenda kinyume na
kifungu cha sheria Na. 140(c) sura ya 16 cha kanuni ya adhabu.
Shija alisisitiza Mama Muddy alitumbukiza dawa za kumfanya binti huyo kuweza
kuhimili vishindo vya mfanyabiashara wakati wa tendo la ngono.
Hakimu Luhwago aliahirisha kesi hiyo hadi Septemba 29 mwaka huu
itakaposikilizwa tena.
0 Comments:
Post a Comment