Tuesday, September 27, 2016

Jela miezi 9 kwa wizi wa simu



ILALA, DAR ES SALAAM
MAHAKAMA ya Mwanzo ya Ilala jijini Dar es Salaam imemhukumu Norman Norvat ‘Nyoka B’(25) kwenda jela miezi tisa kwa kosa la wizi wa simu yenye thamani ya Sh. 180,000.
Ilidaiwa mahakamani hapo na Karani Blanka Shayo kuwa mshtakiwa alitenda kosa hilo Agosti 3 mwaka huu saa 9 usiku katika Mtaa wa Likoma, Kariakoo.
Aidha Shayo alidai siku ya tukio mlalamikaji Pius Alphonce ambaye ni rafiki wa mshtakiwa akiwa na wenzake watatu walilala uani huku simu yake aina OGM ikiwa karibu na mto.
Shayo aliongeza shahidi namba mbili ndiye aliyemuona mshtakiwa akiingia katika nyumba ya mlalamikaji na kutokomea na simu hiyo.
Hakimu Matrona Luanda alisema mahakama kwa pamoja imemtia hatiani ambapo mshtakiwa amehukumiwa adhabu kali ya miezi tisa gerezani baada ya kukiuka sheria za nchi na akimaliza alipe thamani ya simu aliyoiba.

0 Comments:

Post a Comment