Manchester United
itaendelea kusalia kama Mashetani Wekundu au upande wa pili wa Bluu wataweza
kuiba haki hiyo?
Sasa leo (7.1.2020) katika
nusu fainali ya kwanza kutashuhudiwa miamba kutoka jiji la Manchester United
ikipepeta tena katika Kombe la Carabao.
Kikosi cha Ole Gunnar
Solskjaer kilipeleka majonzi katika mchezo uliopita wa Ligi Kuu katika dimba la
Ettihad kwa kuibuka na ushindi wa mabao 2-1; Marcus Rashford na Anthony Martial
wakifanya kazi nzuri.
Manchester United imefika
hapo baada ya kuizabua Rochdale katika mzunguko wa tatu pia kupata ushindi
dhidi Chelsea na Colchester United na kutinga hatua hiyo ni mafanikio makubwa
ikiwa ni mara ya kwanza baada ya kufanya hivyo mwaka 2017 dhidi ya Southampton.
Man City wakiwa mikononi
mwa Pep Guardiola walifika hapo baada ya kuzibamiza Preston North End,
Southampton na Oxford United.
Aidha The Citizens ni
mabingwa watetezi endapo watafanikiwa kutwaa taji hilo tena watakuwa ni timu ya
pili baada ya Liverpool kushinda mataji matatu ya Ligi.
Katika mchezo wa leo
Guardiola atakuwa na mlinzi wake Aymeric Laporte na winga Leroy Sane baada ya
kuwa nje kwa majeruhi licha ya kwamba inaweza ikawa ngumu kuwachezesha wote
wawili katika mzunguko wa kwanza wa nusu fainali hii.
0 Comments:
Post a Comment