Januari 17, 1961 alifariki
dunia mwanasiasa na mwanaharakati aliyepigania uhuru wa taifa la Jamhuri ya
Kidemokrasi ya Kongo (DRC) Patrice Lumumba. Kwa mujibu wa ripoti za Ubelgiji na
Marekani, zilisema kuwa Lumumba alipigwa risasi na kuuawa mnamo saa 3 na dakika
40 usiku.
Ukweli ni kwamba Lumumba
alipata maadui wengi kutokana na kuwa karibu na Urusi, wakati huo wa Vita
Baridi.
Licha ya kupingwa na nchi
za kimagharibi ikiwemo Marekani na Ubelgiji, Lumumba alifanikiwa kuipatia uhuru
Zaire wakati huo ikiitwa Belgian Cong Uhuru Juni 30, 1960 na baada ya hapo
Lumumba akawa waziri mkuu, huku Joseph Kasavubu akiwa raisi wa taifa hilo.
Lumumba ni miongoni mwa
wanaharakati wanaokumbukwa sana katika historia ya dunia kutokana na ujasiri na
msimamo wake katika kumtetea mtu mweusi.
Mnamo Novemba 25, mwaka
1960 akiwa amejificha kwenye kiti cha nyuma cha gari huku mvua kubwa ikinyesha
aliondoka kisiri kwenye makazi yake ili kusaka kuungwa mkono huko kwenye ngome
yake Stanleyville.
Jeshi la Umoja wa Mataifa
halikuruhusiwa kujihusisha na siasa za Congo na hivyo liliagizwa lisijihusishe
na harakati za Lumumba wala wafuasi wake.
Alikamatwa na askari wa
Mobutu na kutiwa korokoroni huko Thysville.
Hata akiwa gerezani,
Lumumba alikuwa tishio kwa Kasa-Vubu,
Mobutu, lakini pia kwa Marekani na Ubelgiji.
Kwa hiyo wakati Katibu mkuu
wa Umoja wa Mataifa Dag Hammarskjöld na wawakilishi wake wakipigania aachiliwe
huru, Kasa-Vubu na Mobutu, kwa usaidizi wa Ubelgiji walikuwa wanasaka mbinu za
kummaliza kabisa.
Hivyo mpango ulisukwa
kumkabidhi Lumumba kwa watu wa Kasai waliotaka kulipiza kisasi.
Ndege ilimchukua Lumumba na
wenzake watatu, ndani ya ndege walipata kipigo na mateso makali na baada ya
kutua Katanga walipelekwa eneo la mafichoni ambako waliuawa na kuzikwa.
Siku iliyofuatia miili yao ilifukuliwa, ilikatwakatwa na kuyeyushwa
kwenye tindikali ya Sulfa.
Mpaka leo hii mabaki ya
miili yao iliko ni kitendawili kisicho na jibu, wakati huo Patrice Lumumba
alikuwa yu ngali kinda mwenye umri wa miaka 36 tu.
Lumumba alikulia katika
familia ya kikatoliki yenye watoto wanne. Alipata elimu ya msingi ya
kiprostestanti na baadae elimu ya sekondari katika shule ya seminari ya kanisa
la katoliki.
Katika maisha yake alifanya
kazi katika shirika la posta kama muuza bia.
Mnamo mwaka 1951 Lumumba
alifanikiwa kupata mke aliyejulikana kwa jina la Pauline Opangu.
Alipokuwa akifanya kazi
katika shirika la Uchapishaji la Ubelgiji mnamo mwaka 1955, alipata tuhuma za
wizi wa fedha na kuhukumiwa kifungo cha miaka miwili, lakini kwa mujibu wa
mwanasheria wa Kibelgiji Lumumba alipunguziwa kifungo badala ya miaka 2
akahukumiwa kwa miezi 12.
Baada ya kutoka jela mnamo
Julai 1956, Lumumba alifanikiwa kuanzisha chama kilichojulikana kama MNC
(Movement National Congolese) na mpaka kufikia mwaka 1958’s Lumumba alikuwa
mwenyekiti wa chama hicho.
Lumumba alikuwa miongoni
mwa watu walioudhuria mkutano wa WATU WOTE WA AFRIKA (ALL AFRICAN PEOPLE)
uliofanyika nchini Ghana mnamo Desemba mwaka 1958, na mwenyeji wake alikuwa
Nkwame Nkurumah.
Umaarufu wake uliibuka
wakati wa sherehe za uhuru wa Congo tarehe 30 Juni 1960 baada ya mfalme Baudoin
wa Ubelgiji kutumia fursa ya sherehe hizo kutetea yale yaliyofanywa na Ubelgiji nchini humo.
Joseph Kasa-Vubu, Rais wa
kwanza wa Congo wakati huo alijibu
hotuba hiyo kwa heshima na taadhima lakini Lumumba alipochukua kipaza sauti
hakusitiri neno.
Akatumbua jipu na kukemea
ukoloni wa wabelgiji akisema ulikuwa ni dhihaka kubwa. Ubelgiji haikutarajia
kwani ilitegemea baada ya uhuru mambo yataendelea kama ada.Siku tano baada ya
uhuru askari wa jeshi la Congo ambalo hakukuwepo na afisa hata mmoja wa
kicongo, wakakengeuka na kuanza kushambulia raia wa kibelgiji.
Ubelgiji ilishindwa
kuchukua hatua huku harakati za kugombea miji mbali mbali zikiendelea.
Ndipo Ubelgiji ikajikita
jimboni Katanga kwenye utajiri mkubwa, jimbo ambalo lilijitenga.
Rais Kasavubu na Waziri
Mkuu wakeLumumba walisaka usaidizi kutoka Marekani kwa Rais Eisenhower bila
mafanikio yoyote na hivyo wakabisha hodi Umoja wa Mataifa.
Baraza la Usalama la Umoja
wa Mataifa likaidhinisha kupelekwa kwa kikosi kikubwa cha walinda amani ili
kuoondoa askari wa kibelgiji huko Congo na kurejesha utulivu wa raia na
utawala.
Kikosi cha kwanza cha
askari 3,000 kutoka nchi za Afrika kiliwasili ndani ya siku tatu, na wengine 10,000 waliwasili wiki mbili
baadaye kukiwa na watendaji ili kuondoa pengo la utawala wa raia, huduma za
afya, mawasiliano na usalama.
Nia ikiwa kuelekeza
wanaCongo jinsi ya kuongoza nchi yao.
Mpaka sasa Patrice Lumumba
anakumbukwa na watu wengi hapa duniani kwa kuwa mstari wa mbele katika ukombozi
wa mtu mweusi juu ya utawala wa kikoloni.
Kwani kuna barabara
zinatumia jina la Lumumba, kuna Mitaaa inatumia jina la Lumumba, kuna Nyimbo
ziliitwa Lumumba, kuna Makundi ya wasanii yanatumia jina la Lumumba, kuna kumbi
za mikutano na vyuo na taasisi mbalimbali zinatumia jina la Lumumba.
Hakika jina la Lumumba
halitasahaulika katika Historia ya Ulimwengu huu hususani barani Afrika.
Katanga ilijitenga,
wanajeshi wa kibelgiji wakiendelea kuwepo huku vikosi vya Umoja wa Mataifa
vikiwa havina mamlaka ya kuwashambulia bali kuweka majadiliano. Lumumba
hakufurahi Alisaka usahiba na Urusi huku vyombo vya habari vya magharibi
vikidai ni kibaraka wa nchi hiyo, jambo ambalo baadaye lilimchochea kusaka
usaidizi wa kijeshi kutoka Urusi ambapo ndege 11 za mizigo ziliwasili
Stanleyville zikiwa na bendera ya Congo na zimeandikwa Jamhuri ya Congo.
Lumumba hata alitishia
kufukuza kikosi cha Umoja wa Mataifa na yaelezwa kuwa mapema mwezi Septemba
baada kuomba usaidizi wa kijeshi kutoka Urusi, shirika la ujasusi la
kimarekani, CIA lilipatiwa kibali kumuua, lakini walishindwa wakati huu
kutokana na ulinzi mkali kutoka Umoja wa Mataifa.
Lumumba alisaka kumaliza
harakati za kujitenga kwa jimbo la Kasai.
Alibeba askari kwa kutumia
ndege za kisovieti kwenda Katanga ambapo askari walijitwalia madaraka na hata
kuripotiwa vitendo vya ubakaji na uporaji kwa watu wa jamii ya Luba.
Hii ilimjengea uadui
mkubwa. Kitendo hiki kilimchochea Rais Kasa-Vubu na kwa ushawishi wa Marekani,
alimuondoa Lumumba serikalini kwa madai ya kutumbukiza taifa kwenye vita vya
wenyewe kwa wenyewe.
Lumumba alijibu hoja
kupitia redioni na kutoa wito kwa wananchi wa Congo kusimama kidete na
kupambana ili wafe nae.
Kwa kuwa nchi za magharibi
zilimuunga mkono Rais Kasavubu huku Urusi ikimuunga mkono Lumumba , Congo
iligawanyika pande mbili, Mashariki na Magharibi huku Umoja wa Mataifa ukiwa
kati. Siku chache baadaye mambo yalibadilika baada ya mnadhimu mkuu wa Lumumba, Kanali Joseph Mobutu
alipohamia upande wa pili.
Kufuatia
ushawishi wa Marekani, Mobutu alitangaza kupitia radio kuwa anachukua serikali
akiwa mrengo wa Rais Kasavubu na kuwa kiongozi mkuu wa serikali.
Lumumba, akiwa chini ya ulinzi wa vikosi vya Umoja wa Mataifa
aliendelea kuishi akiwa ametengwa kwenye makazi ya Waziri Mkuu lakini zama zake
za utawala zimefika ukingoni.
Pindi Baraza Kuu la Umoja
wa Mataifa lilipolazimika chini ya shinikizo la Marekani kupiga kura kumtambua
Kasa-Vubu na Mobutu kuwa wakaliaji halali wa kiti cha Congo kwenye Baraza Kuu
la Umoja huo, ndipo Lumumba alitambua kama karata kishalamba garasa mchezo
umekwisha.
Alizaliwa Julai 2, 1925,
huko Onaluwa, Katako-Kombe katika mkoa wa Kasai.
0 Comments:
Post a Comment