Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania John Magufuli amemfuta kazi Waziri wa Mambo ya Ndani wa nchi hiyo
Kangi Lugola, akisema wizara hiyo inaongoza katika kuchukua miradi ya ovyo.
Rais Magufuli pia amemfuta
kazi Kamishna wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji nchini humo, Thobias Andengenye
kwa kusimamia mradi usieleweke wenye thamani ya dola za kimarekani milioni 452.
Rais Magufuli alitangaza
kuwafuta kazi viongozi hao wawili muda mfupi baada ya kuzindua mradi wa nyumba
za maofisa magereza katika mji wa kibiashara wa Dar es Salaam.
Amesema naibu waziri wa
Mambo ya Ndani Hamad Masauni na katibu mkuu wa wizara hiyo Jacob Kingu
wamemwandikia barua ya kujiuzulu nyadhifa zao na amezipokea.
George Simbachawene aliyekuwa
Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira amechukua nafasi ya Kangi Lugola.
Simbachawene anakuwa waziri wa 26 kuchukua nafasi hiyo tangu mwaka 1961. Pia wizara
ya Mambo ya ndani ndiyo wizara ngumu nchini.
0 Comments:
Post a Comment