Monday, January 6, 2020

Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs) ni nini?


Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs) ni seti ya malengo 17 ya ulimwengu ambayo yamedhamiria kuubadilisha ulimwengu kutoka katika hali yake ya sasa ambayo imejaa umaskini wa kutisha, changamoto ya njaa, mabadiliko ya tabia ya nchi, uhaba na ubovu wa huduma za msingi za jamii kama vile elimu na afya, machafuko na ghasia, uchumi husio jumuishi, na matatizo ya ajira na kazi zisizo za staha, kwenda kwenye ulimwengu ambao utakuwa hauna aina zote za umaskini, ulimwengu wenye chakula cha kutosha, huduma nzuri za afya, elimu, maji, nishati, miundombinu ya usafirishaji, usawa wa kijinsia, na haki na usawa kwa jamii.

Malengo 17 ya Maendeleo Endelevu
Orodha ya malengo 17 ya maendeleo endelevu ni pamoja na:
1. Kutokomeza umaskini,
2. Kukomesha njaa,
3. Afya njema na ustawi,
4. Elimu bora,
5. Usawa wa kijinsia,
6. Maji salama na usafi,
7. Nishati mbadala kwa gharama nafuu,
8. Kazi zenye staha na ukuzaji uchumi,
9. Viwanda, ubunifu na miundombinu,
10. Kupunguza tofauti,
11. Miji na jamii endelevu,
12. Matumizi na uzalishaji wenye uwajibikaji,
13. Kuchukua hatua dhidi ya mabadiliko ya tabia ya nchi,
14. Kuendeleza uhai katika maji,
15. Kulinda uhai katika ardhi,
16. Amani, haki na taasisi madhubuti,
17. Ushirikiano ili kufanikisha malengo.

0 Comments:

Post a Comment