Katika siku ya kwanza ya Dakar Rally 2020 katika jangwa la
Saudia hapo jana Januari 5 kumeshuhudiwa dereva wa magari ya kampuni ya Mini
Vaidotas Zala aliustaajabisha ulimwengu baada ya kumaliza nafasi ya kwanza
katika hatua ya kwanza ambayo ilianza Jeddah hadi Al Wajh.
Ushindi huo umempiku bingwa mtetezi wa mbio hizo katika magari Nasser Al-Attiyah ambaye hapo
jana aliongoza lakini pancha tatu alizopata katika safari hizo zilitoa mwanya
kwa Zala mwenye umri wa miaka 32 raia wa Lithuania.
Zala alitumia saa 3:19:04 huku nafasi ya pili ikishikwa na
dereva mwingine wa mini Stephane Peterhansel (54) wa Ufaransa kwa saa 3:21:18.
Nafasi ya tatu ilishikwa na dereva kutoka Hispania Carlos
Sainz akitumia saa 3:21:54 huku Al-Attiyah alishika nafasi ya nne akitumia saa
3:24:37.
Kwa upande wa malori kulishuhudiwa dereva wa kampuni ya
malori ya Kamaz ya Russia Anton Shibalov
akimpita dereva mwenzake Andrey Karginov ambaye alishika nafasi ya saba.
Bingwa mtetezi wa mbio hizo katika kategori hiyo Eduard
Nikolaev alishika nafasi ya 10 akipoteza dakika 11 kutoka kwa mshindi wa hatua
hiyo Shibalov.
Nafasi ya pili ilishikwa na dereva wa kampuni ya Maz ya Belarus
Siarhei Viazovich na Janus van Kasteren wa kampuni ya De Rooy Iveco alishika
nafasi ya tatu.
0 Comments:
Post a Comment