Januari 7, 2017 alifariki
dunia mwanasiasa wa Ureno Mario Soares ambaye aliwahi kulitumikia taifa hilo
kama Waziri Mkuu na raia wa 17 wa Ureno.
Jina lake halisi ni Mario Alberto Nobre Lopes Soares. Alikuwa Waziri Mkuu wa
Ureno kutoka mwaka 1976 hadi mwaka 1978 na pia mwaka 1983 hadi mwaka 1985.
Alishika madaraka ya kuliongoza taifa hilo kama rais wa 17 mnamo mwaka 1986
hadi mwaka 1996.
Aidha Soares alikuwa Katibu Mkuu wa kwanza wa Chama cha
Socialist tangu kuanzishwa kwake mnamo mwaka 1973 hadi mwaka 1986.
Kifo cha
mwanasiasa huyo mashuhuri nchini Ureno kilikuwa hivi, alipelekwa hospitali
Desemba 13, 2016 licha ya hali yake ya kiafya kuonyesha kwamba alikuwa ahueni.
Siku 13 baadaye yaani siku ya Boxing ya Desemba 26 alishindwa kabisa kuendelea
kuhimili kwani uwezo wake wa mwili kuendelea kufanya kazi kwa ufanisi
ilishindikana.
Baada ya kifo chake Januari 7, 2017 Serikali ya Ureno ilitangaza
siku tatu za maombolezo ikiwa ni mara ya kwanza tangu mwaka 1951 ilipofanyika
hivyo kwa miongoni mwa marais waliowahi kutawala taifa hilo Oscar Carmona.
Ibada
ya mazishi ilifanyika katika jumba la Jeronimos mnamo Januari 9, 2017 na Soares
alizikwa katika makaburi ya Prazeres katika siku inayofuata karibu na kaburi la
mke wake.
Mwanasiasa huyo ni mtoto wa João Lopes Soares (1879-1970) ambaye ni
mwanzilishi wa Chuo cha Moderno kilichopo jijini Lisbon. Baba yake huyo alikuwa
waziri wa serikali na baadaye kuwa mwanaharakati aliyepinga utawala wa
kifashisti.
Awali baba yake huyo alikuwa kiongozi wa dini kabla hajampa
ujauzito Elisa Nobre Baptista (1887-1955) ambaye alikuja kumzaa Soares.
Pia
Mzee Soares alikuwa mtoto mwingine ambaye hakuwa anafahamika sana Tertuliano
Lopes Soares.
Mario Soares alikulia katika kanisa Katoliki, lakini
alijipambanua katika siku za usoni kuwa yeye ni Mjamaa, asiyependa dini
kuingilia masuala ya serikali na aliyependelea nchi kuwa katika mfumo wa
Jamhuri.
Soares alizaliwa katika viunga vya Coração de Jesus jijini Lisbon na
alifanikiwa kuhitimu katika masuala ya historia na falsafa katika Chuo Kikuu
cha Lisbon.
Mnamo mwaka 1957 alipata kuwa mhadhiri wa Chuo Kikuu na akiwa
katika nafasi hiyo alikuwa akienda kinyume na udikteta wa Antonio de Oliviera
Salazar ambaye alikuwa akiongoza taifa hilo hali iliyomfanya awe anakamatwa
mara kwa mara.
Pia Soares alikuwa pamoja na vikundi vya wanaharakati waliopinga
ufashisti na kuitaka demokrasia. Pia Soares alisoma masomo yake katika chuo kilichokuwa
kikimilikiwa na baba yake cha Moderno.
Akiwa hapo Moderno alifundishwa Jiografia
na Alvaro Cunhal alikuwa mwaka wake. Akiwa mwanafunzi wa chuo kikuu Soares
alijiunga na Chama cha Kikomunisti cha Ureno katika idara ya vijana.
Akiwa katika
idara hiyo aliunda maandamano jijini Lisbon kwa ajili ya kusherekea mwisho wa
vita vya pili vya dunia.
Alikamatwa na maofisa wa Jeshi la Polisi la Ureno mnamo
mwaka 1946 wakati akiwa ni mjumbe wa Kamati Kuu ya chama cha Movimento de
Unidade Democrática wakati mwenyekiti wake wakati huo akiwa ni Mário de Azevedo
Gomes.
Pia mwaka 1949 Soares alikamatwa mara mbili na Jeshi la Polisi wakati
huo akiwa ni Katibu wa Mwanasiasa Norton de Matos aliyekuwa akiwania urais wa
taifa hilo.
Februari 22, 1949 alimwoa
mwigizaji Maria de Jesus Barroso Soares wakati huo akiwa jela ya Aljube na
baadaye walifanikiwa kupata mtoto aliyefahamika kwa jina la João Soares ambaye
baadaye alikuja kuwa meya wa jiji la Lisbon.
Pia mwaka 1951 walimzaa mtoto
mwingine wa kike waliyempa jina la Isabel Barroso Soares ambaye kwa sasa (2019)
anasimamia chuo hicho cha Moderno.
Kutokana na kukamatwa kila wakati na Jeshi
la Polisi kuliifanya kazi yake ya uhadhiri wa Historia na Falsafa kuwa ngumu
hivyo aliamua kusomea Sheria na baadaye alikuja kuwa Mwanasheria.
Mnamo mwaka
1970 alikimbilia uhamishoni Rome, Italia licha ya kwanza baadaye alikwenda
kuishi zake Ufaransa ambako alisoma katika vyuo vitatu vya Vincennes, Paris na
Rennes.
Alichaguliwa kuwa Katibu Mkuu wa chama cha Socialist baada ya
Portuguese Socialist Action kuwa chama. Chama hicho kiliundwa chini ya mwavuli
wa Willy Brandit wa chama cha SPD nchini Ujerumani Aprili 19, 1973.
Utawala wa
Salazar uliendelea kutowafurahisha watu wa Ureno ambapo Aprili 25, 1974 jeshi
la Ureno lilikamata jiji la Lisbon na taifa hilo kuwa mikononi mwa Marcelo
Caetano.
Soares na wanasiasa wengine waliokuwa uhamishoni walirudi Ureno kwa
ajili ya kusherekea kwa kile walichokiita Mapinduzi ya Carnation baada ya
kuuangusha utawala wa Salazar.
Mnamo mwaka
1976 kulifanyika uchaguzi wa bunge ambao uliwapa Socialist uwingi wa viti ambao
uliwafanya kuunda upya na ndipo Soares alipochaguliwa kuwa Waziri Mkuu.
Uhasama
mkubwa baina ya Wajamaa na Wakomunisti ulisababisha serikali ya mrengo wa shoto
kushindikana hivyo Soares aliunda serikali dhaifu ya wachache ambayo haikumpa
kuwa maarufu hivyo mnamo mwaka 1978 alijiuzulu.
Katika uchaguzi mkuu wa mwaka
1986 alichaguliwa kuwa Rais wa Ureno akimshinda Diogo Feitas do Amaral kwa
asilimia mbili tu.
Pia akachaguliwa tena mwaka 1991 na wakati huo asilimia 70
ya kura. Kwa kipindi chote Soares alipokuwa madarakani aliiongoza Ureno katika
siasa za kidemorasia za mrengo wa kati kulia chini ya chama cha Social
Demokratic kilichokuwa mikononi mwa mwenyekiti AnÃbal Cavaco Silva.
Soares alifariki dunia
akiwa na umri wa miaka 92 alizaliwa Desemba 7, 1924.
0 Comments:
Post a Comment