Mshikiliaji rekodi ya dunia mbio za marathon, Eliud Kipchoge amebeza uzushi wa mahasidi wake ambao walikuwa wanazua kuwa rekodi yake ya kumaliza mbio za marathon chini ya saa mbili ilichangiwa na viatu vyake vya Nike.
Asasi za riadha zinapania kufanya mkutano na wakufunzi hao wenye utata pamoja na wapinzani wa Nike kwa kusema kuwa wanatakiwa kupigwa marufuku. Kipchoge, alisema hamna haja ya masharti makali kwani spoti yatakiwa kukumbatia teknolojia.
Akitolea mfano wa Formula 1, alisema Pirelli ndio hutengeneza magurudumu ya magari yote lakini Mercedes ndio bora.
Kwa sababu ya injini. Hivyo amesisitiza kuwa mtu binafsi ndiye hukimbia bali sio viatu. Viatu hivyo vya Nike Vaporfly, havikuwa sababu mojawapo ya rekodi ya Kipchoge kukosa kutambuliwa na Shirikisho la Riadha Duniani (IAAF).
Wakati huohuo mkimbiaji mwenye kasi namba mbili wa marathon Kenenisa Bekele atakabiliana na Eliud Kipchoge katika Marathon ya London mwezi Aprili.
Muethiopian huyo mwenye miaka, 37, alikuwa nyuma ya Kipchoge kwa sekunde mbili tu aliyeweka rikodi katika marathon ya Berlin.
CHANZO: CRI Swahili
0 Comments:
Post a Comment