Januari
20, 1974 timu za nchini Uingereza kwa mara ya kwanza zilikutana katika mchezo
wa ligi katika siku ya Jumapili.
Timu hizo ni Fulham na Milwall ndizo
zilizoweka rekodi hiyo ya kwanza. Chama cha Soka cha England (FA), klabu
mbalimbali na wachezaji walionyesha kuunga mkono wazo la kwamba mechi
zikichezwa siku ya Jumapili, zitapunguza mashabiki na mapato katika viwanja.
Sheria
ambayo ilikuwa ikijulikana kama The Sunday Observances Act ya mwaka 1695 ilikuwa
ikizua matukio siku ya Jumapili ili kuwapa muda wanaoenda kanisani.
Sheria hiyo
ilikuwa ikizua kuuzwa kwa tiketi siku ya Jumapili. Hata hadhira ya watu
ilipinga kwa kiasi kikubwa siku ya Jumapili kufanyika au kuchezwa mechi yoyote.
Lakini Januari ya mwaka 1974 mahudhurio yaliendelea kupungua lakini chama cha
soka nchini humo kiliendelea kupambana katika Kombe la FA mzunguko wa nne na
watatu siku ya Jumapili.
Kwa kubadilisha program zao kuliivutia kamati ya
mashindano ya Ligi kutokana na mechi za Kombe la FA zilikuwa na mvuto na wengi
walijaa bila kujali kuwa ni Jumapili.
Klabu za Ligi Kuu wakati huo First
Division zilikataa kabisa kucheza Jumapili kwa kigezo cha dini.
Ligi daraja la
kwanza zilifanikiwa kuandaa mechi 12, Ligi daraja la pili na la tatu ziliandaa
mechi mbili, Ligi daraja la nne zilifanikiwa kuandaa mechi sita.
Katika mechi
hizo kuliripotiwa kuwa michezo tisa ilijaza watu wa kutosha tofauti na
matarajio.
Licha ya mafanikio hayo siku ya jumapili iliendelea kupata upinzani
mkali hadi pale ailipokuja kurasimishwa. Sasa basi mchezaji wa Millwall Brian
Clark aliweka historia ya kwanza kwa kufunga bao la kwanza siku ya Jumapili katika
mfumo huo mpya kwenye mchezo dhidi ya Fulham.
Brian Clark alizaliwa Januari 13,
1943 mjini Bristol na kufariki dunia akiwa na umri wa miaka 56 hiyo ilikuwa
Agosti 10, 2010 jijini Cardiff.
Brian Clark anakumbukwa pia kwa bao pekee
alilofunga akiwa na Cardiff City dhidi ya Real Madrid katika mzunguko wa kwanza
hatua ya robo fainali ya Kombe la Washindi barani Ulaya mnamo mwaka 1971.
0 Comments:
Post a Comment